Tangakumekuchablog
MKUU wa
Mkoa wa Tanga, Said Magalula amevilaumu vyombo vya habari kulishabikia tukio la
Amboni Tanga na kulita la Kigaidi jambo
ambalo limeleta taswira mbaya Kimkoa na Kitaifa.
Akizungumza
na waandishi wa habarui jioni hii mjini Tanga, Magalula alisema vyombo hivyo
vimeipotosha umma na hivyo kuvitaka kutumia weledi wao wa upashaji habari na
kuacha kutumia uhuru wa habari vibaya.
Alisema
Tukio hilo limekuwa gumzo Tanzania mzima na kuonekana Tanga imevamiwa na
kikundi cha Al Shaabab jambo ambalo halina ukweli wowote.
“Kwa siku
mbili mfululizo tumeona baadhi ya vyombo vya habari kuripoti tukio kinyume na
lilivyo ----kwa kweli limenihuzunisha sana” alisema
“Ukweli wa
tukio lile ni la ujambazi ambao walikuwa wakiteka magari na unyan’anyi katika
magadouni na na kuficha kule mapangoni---tukimaliza hapa nawaomba sote kwa
pamoja twende katika tukio tukashuhudie” alisema Mgalula
Mgalula
amevitaka vyombo vya habari kuitumia taaluma yao katika kuandika ukweli na
kuacha kuipotosha jamii na kuwaweka katika vitisho na kusababisha kuporomoka
maendeleo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment