Wednesday, February 11, 2015

MWIZI ANAPOINGIA NDANI NA KUKUTANA NA KITICHA CHA PESA KIKIWA NA UJUMBE

Hivi unaweza kuacha CASH mezani kwako na ujumbe eti mwizi akiingia azichukue? Isome hii…

Masked
Hakuna mtu anayependa uhalifu hata kidogo, lakini vipi unakutana na mtu ambaye anaacha pesa ndani ya nyumba yake pamoja na ujumbe kwa mwizi yoyote ikitokea kaingia ndani ya nyumba basi ajichukulie kiurahisi!
Nakusogezea kutoka China, wanandoa wameacha hela kwenye meza kiasi cha Yuan 300 (sawa na sh. elfu 85 Tshs) pamoja na ujumbe ambao unamtaarifu mwizi yoyote atakayeingia achukue hela hizo.
Imekuwa kawaida yao kufanya hivyo, safari hii walikuwa wakisafiri kwenda Shenzhen, Kusini mwa China safari ambayo walipanga kukaa kwa miezi miwili.
Ujumbe waliouacha unasomeka hivi; “Najua umehangaika sana mwaka huu. Lazima una hamu ya kuwaona wazazi wako, chukua pesa hizi kakate ticket ya treni na uende kuwasalimia. Kama ukirudi utafute kazi ya heshima
7427ea210acc164536a12b
Ujumbe wa wanandoa hao pamoja na cash waliyoiacha kwenye meza yao.
Mwaka 2010 waliwahi kusafiri na kuacha pesa na ujumbe kama huo, waliporudi walikuta mlango umevunjwa na pesa zimeibiwa lakini hakuna kitu chochote kingine ambacho kimeibiwa ndani ya nyumba yao.
Hautopitwa na story yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment