P.Diddy matatani kwa kupigana.
Rapa maarufu na mmiliki wa Lebo ya Bad Boy Entertainment Sean Combs maarufu kama P Diddy anasakwa na polisi kwa madai ya kumpiga shabiki mmoja katika hafla ya mchezo wa Super Bowl iliyofanyika nchini Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita .
Kwa mujibu wa mitandao kadhaa ikiwemo TMZ , mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Steven Donaldson ambaye ana umri wa miaka 45 alipigwa ana mtu anayedhaniwa kuwa P Didy katika hafla ya Super Bowl iliyofanyika jumamosi usiku .
Mkanda mmoja wa video unamuonyesha Didy akibishana na mtu huyo wakiwa wanatazamana uso kwa uso katika tukio ambalo Diddy anadaiwa kumpiga usoni kitendo ambcho hata hivyo hakikuonekana kwenye mkanda huo .
Steven Donaldson anadai kuwa Didy alimpiga usoni kabla ya kuwaagiza walinzi wa hafla hiyo kumtoa nje huku yeye (Diddy) akibakia kwenye eneo la tukio .
Stevn aliishia kufungua mashtaka dhidi ya Diddy ambapo Polisi walifika eneo la tukio lakini hawakuweza kumkua nyota huyo kwani alikuwa ameondoka .
Polisi nwa eneo la Scotsdale wamesema kuwa wanamtafuta Diddy ili wamhoji kuhusuaina na tukio hilo na waweze kupata upande wake kabla ya kuamua kama atakuwa na shitaka la kujibu au la .
Chanzo cha ugomvi huo kinadaiwa kuwa malalamiko ambayo Stevn aliyatoa baada ya kulipa kiingilio cha dola mia moja ili amuone P Diddy lakini star huyo hakujichanganya na watu wengine ambapo aliishia kukaa kwenye eneo la VIP .
Hii itakuwa mara ya pili kwa Diddy kukumbwa na tukio kama hili baada ya kudaiwa kumpiga ngumi rapa wa lebo ya Cash Money Drake kwenye klabu moja ya usiku huko Miami baada ya kutokea ubishi baina ya wasanii hao juu ya haki miliki ya wimbo .
No comments:
Post a Comment