Kutana na list ya vyakula ambavyo vinatoa harufu mwilini.
Moja kati ya vyakula vinavyomletea mlaji wake harufu kali ni vitunguu swaumu ambavyo hutumika kama viungo kwenye chakula .
Vitunguu swaumu vina vitu Fulani ndani yake ambavyo hujitokeza pale kinapokatwa , kusagwa au hata kutafunwa vitu hivi kitaalamu hufahamika kama Allicin na Allin na hivi ndio hasa husababisha harufu kali ambayo hutokea baada ya mtu kula vitunguu swaumu au vyakula vilivyoungwa kutumia vitunguu swaumu .
Pamoja na hayo vitunguu swaumu vina faida kubwa sana mwili mwa mwanadamu na faida hizo huletwa na hii Illin ambayo inatajwa kuwa sababu ya harufu yake mbaya na moja kati ya faida zake ni jinsi ambavyo vitunguu swaumu husaidia kupambana na bacteria wanaoleta magonnjwa mbalimbali na virusi tofauti .
Mbegu ya Binzari
Mbegu ya Binzari hutumika kwenye mapishi ambapo huleta ladha nzuri kwenye chakula , hata hivyo mbegu hizi husababisha harufu mbaya ambayo inabakia mdomoni kwa muda mrefu . Kama unataka kupunguza harufu mbaya unaweza kuipunguza kwa kunywa maji mengi na kutumia vyakula vingine ambavyo vinatumika kupunguza harufu ambavyo havina harufu kali .
Nyama nyekundu ni moja kati ya vcyakula vinavyosababisha harufu mbaya mdomoni na tumboni . Ni vigumu kwa watu wengi kukubaliana na hili kwa kua nyama nyekundu ni moja kati ya vyakula vinavyopendwa sana na watu . Tafiti zinaonyesha kuwa jasho jingi ambalo husababishwa na mafuta yanayoganda mwilini kutokana na ulaji wa nyama nyekundu ni moja kati ya vitu ambavyo huleta harufu mbaya kwenye mwili wa mwanadamu .
Nyama nyekundu ni moja kati ya vyakula sugu kwa kusababisha harufu mbaya mdomoni na inayotokea tumboni .
Mboga Za Majani
Baadhi ya mboga za majani zinasababisha harufu mbaya mwilini nazo ni cauliflower , kabichi, broccoli na nyinginezo nyingi .
Kahawa
Kahawa nayo iko kwenye orodha ya vyakula ambavyo vinasababisha harufu mbaya mdomoni na mwilini kwa jumla . Moja vitu ambavyo vimo ndani ya kahawa ambavyo ni Caffeine husisimua mfumo wa neva yaani ile mishipa ya fahamu mwilini na husababisha mtu avuje jasho kwa wingi kuliko kawaida .
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment