Mkusanyiko wa stori kubwa zilizopewa headlines kwenye Magazeti ya leo February 6, 2015 ziko hapa
MWANANCHI
Kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kuwa wanafunzi walioshiriki gwaride na halaiki kwenye sherehe za miaka
38 ya CCM mjini Songea ni watoto wa wanachama wa chama hicho,
imekosolewa na wananchi na wabunge ambao walifikia uamuzi wa kuomba
mwongozo.
Sherehe hizo zilifanyika Jumapili ya
Februari Mosi kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, zikishirikisha
makundi mbalimbali, wakiwamo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
ambao walivalia sare za CCM na kuimba nyimbo za chama hicho huku
wakicheza gwaride na halaiki, ambayo kwa kawaida huchukua muda mrefu
kujifunza na kuielewa.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo,
mtendaji huyo mkuu wa Serikali alitetea ushiriki wa watoto hao wapatao
500 kwenye sherehe hizo akisema ni sehemu ya mfumo wa wanachama wa CCM.
“Susan,
utafikiri tulikuwa pamoja. Nilijua tu swali hili lazima litaulizwa. Ila
‘mtoto wa nyoka ni nyoka’. Chama hiki kina mfumo wake ambao umeshuka
mpaka kwenye ngazi ya kitu kinaitwa chipukizi,” alisema
akijibu swali la mbunge huyo aliyetaka kujua sababu za CCM kutumia
watoto kwenye shughuli zake za siasa wakati ina wanachama wapatao
milioni 10 kote nchini.
“Chipukizi
hawa ni watoto ambao wamezaliwa kutokana na wazazi wana-CCM, ndiyo
maana chama kiliwatumia. Sherehe ilikuwa nzuri na ilipendeza sana. Kwa
kuwa hawajafikia umri wa kuingia katika masuala ya siasa, halina madhara
lile rafiki yangu, pia bado ni wadogo mno na walikuwa wanafurahia
gwaride na kuvaa sare tu:-Pinda
MWANANCHIZiara ya rais wa Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck imeacha mjadala mzito kisiwani hapa kutokana na kitendo chake cha kutumia usafiri wa boti kuja Unguja na kutembea kwa miguu hadi Hoteli ya Serena ya Zanzibar.
Rais huyo, akiwa na mwenyeji wake, Dk Ali Mohamed Shein, alikuwa akitembea mitaa ya Mji Mkongwe, huku akisalimiana na wananchi waliokuwa pembeni ya barabara kushuhudia ujio wake.
Tofauti na viongozi wengi wa juu, Rais Gauck alisafiri kutoka Dar es Salaam kwa kutumia boti ya Kilimanjaro 4 na kuwasili saa 5:30 asubuhi na alipokewa na mwenyeji wake, Shein pamoja na wananchi wakiwamo na wanafunzi.
Baada ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride maalum la heshima, kiongozi huyo alianza kutembea huku akisalimia wananchi na wengine kudiriki kuwashika mikono.
Akiwa katika ulinzi wa kawaida, alipita mitaa ya Malindi, Mizigani na Forodhani ambako wananchi walikuwa wamejipanga pembeni huku wakicheza ngoma ya Beni. Siku hiyo maduka yalifungwa kutokana na sababu za kiusalama.
NIPASHE
Wanawake wajane ambao ni Wafugaji jamii
ya Kimasai, wamejikuta wakiangua kilio katika kituo cha Polisi Mvomero,
mkoani Morogoro baada ya kukabidhiwa idadi pungufu ya ng’ombe
zilizokamatwa baada ya kuporwa na kundi la ulinzi wa jadi la wakulima.
Walinzi hao wa jadi kutoka katika kijiji cha Dihombo,
lilivamia Kijiji cha Kambala ambacho wanaishi wafugaji hao na kupora
ng’ombe 145 kwa madai kuwa wafugaji wa kijiji hicho kuwapora wakulima
wenzao pikipiki tatu na kusababisha uhalibifu wa trekta wakati
wakielekea shambani katika bonde la Mgongola na pikipiki hizo
kutelekezwa porini.
Mmoja wa wanawake hao, Belitha William,
alisema akiwa kijijini Kambala akiendelea na shughuli za kuchunga
mifugo yake, ghafla alivamiwa na kundi la vijana wenye silaha za jadi
maarufu kama muano na kupora ng’ombe wake wapatao 145 pamoja na ndama na
kuondoka nao.
Mfugaji huyo alisema alipoifuatilia
mifugo hiyo alielezwa inalindwa na kundi la walinzi wa jadi mpaka pale
wafugaji wa jamii hiyo ya kimasai watakaporudisha pikipiki walizopora
wafugaji wenzao.
Hata hivyo, alisema baadaye mifugo hiyo
ilipelekwa ofisi ya Tarafa ya Mvomero kwa ajili ya kupigwa faini mifugo
hiyo kuzurura katika mashamba huku mingine ikiwa haipo.
Kwa upande wao, wakulima walioporwa pikipiki hizo, Fabian Clement pamoja na Francis Boniface,
wakielezea tukio la kuporwa pikipiki hizo, walisema kwa nyakati tofauti
kuwa wakati wakielekea katika mashamba ya bonde la Mgongola kwajili ya
kuwapelekea chakula wenzao, waliona kundi kubwa la wafugaji jamii ya
Wamasai wakiwa na silaha za jadi pamoja na bunduki likiwafuata ndipo
walipokimbilia porini.
MTANZANIA
Wazir Mkuu wa Zamani Edward Lowassa, amekanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti moja la kila wiki iliyosema “Lowassa apanga safu”, akisema hana haja ya kufanya hivyo wala kutumia fedha kumnadi mgombea yeyote.
Taarifa iliyotolewa ofisi yaje jana,
ilisema habari hiyo ilijengwa na taswira ya uongo kwamba kuna mpango wa
kupanga nani atagombea ubunge katika Jimbo la Monduli baada ya Lowassa
kumaliza muda wake.
“Taarifa hiyo potofu ilikuwa na lengo la kumshushia Lowassa hadhi kwa wananchi wake,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Lowassa anatarajia kupeleka malalamiko rasmi kwenye Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Idara ya Habari (Maelezo) ili ukweli ujulikane.
Ilisema habari hiyo ilidai kuwa Lowassa
amewahonga makada kadhaa wa CCM wilayani humo ambao wameonyesha au wana
nia ya kuwania kiti hicho, Sh millioni 10 kila mmoja ili wamuunge mkono
Mbunge wa Viti Maalum, Namelok Sokoine.
MTANZANIA
Mtuhumiwa Tissi Mallya ambaye alitoroka baada ya kumuua polisi, G.7168 Koplo Joseph Swai, ameauwa usiku wa kuamkia jana na wananchi alipokuwa amejificha akiwa na panga lenye damu lililotumika kwenye mauaji hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime alisema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Mauaji hayo yalitokea juzi asubuhi katika eneo la Chang’ombe Juu.
Kamanda Misime alisema baada ya Malya
kutekeleza mauaji hayo alikimbia lakini ilipofika saa 5.00 usiku
wananchi walimuona maeneo ya Mtimkavu Mailimbili akiwa bado na panga
alilotumia kumuua Koplo Joseph.
“Wananchi
walichukua sheria mkononi na kumshambulia hadi polisi walipofika eneo
la tukio wakamchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Dodoma lakini aligundulika tayari amekwisha kufariki dunia:-Misime
HABARILEO
TANI 200,000 za silaha haramu zilizokuwa zimezagaa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) zimeteketezwa.
Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa EAC, Richard Sezibera mbele ya Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck wakati alipozuru makao makuu ya jumuiya hiyo, jana.
Alisema silaha hizo zilizokamatwa kwa nyakati tofauti katika nchi mbalimbali za EAC ni pamoja na mabomu tani 200.
Akizungumzia ujio wa Rais wa Ujermani
katika makao makuu ya Jumuiya hiyo, Sezibera alikiri kufurahishwa na
ujio huo na kusema kuwa utaongeza chachu ya nchi hiyo kuisaidia jumuiya
hiyo.
Sezibera alisema mahitaji makubwa
yanahitajika katika kufanikisha mahitaji ya wananchi wa EAC ikiwa ni
pamoja na Afya, Mazingira, Miundombinu na vikundi vya akina mama na
vijana wanachama wa jumuiya hiyo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment