FEB8 kwenye kilichoandikwa MAGAZETINI T’zania leo, Kuna hizi story kubwa TANO…
NIPASHE
Moto ambao chanzo chake hakijafahamika, umewateketeza ndugu sita wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Profesa Mark Mwandosya
usiku wa kuamkia jana eneo la Kipunguni A, Dar es Salaam katika nyumba
waliyokuwa wakiishi familia hiyo pamoja na kuteketeza kila kitu
kilichokuwepo ndani ya nyumba hiyo.
Waliofariki katika tukio hilo, dada wa Profesa Mwandosya, Celine Egela (50), mume wake Kapteni mstaafu wa Jeshi, David Mpira (60) mdogo wake Samuel Egela (30), wengine ni mtoto wa dada yake Mwandosya, Lucas Mpira (20) pamoja na wajukuu wawili, Celine Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili na Pauline Emmanuel (5).
Walioshuhudia tukio hilo, wamesema moto huo uliibuka wakati familia hiyo ikiwa imelala ambapo
Josephat Mwakasita, amesema alikuwa mtu wa kwanza kufika eneo hilo baada ya kusikia sauti ya vilio vya watoto wakiomba msaada kutoka ndani ya nyumba hiyo, alipofika eneo hilo alikuta moto ukiwa tayari umetanda nyumba hiyo.
Josephat Mwakasita, amesema alikuwa mtu wa kwanza kufika eneo hilo baada ya kusikia sauti ya vilio vya watoto wakiomba msaada kutoka ndani ya nyumba hiyo, alipofika eneo hilo alikuta moto ukiwa tayari umetanda nyumba hiyo.
“Nilishindwa
kuingia kuwaokoa majirani zangu, niliomba msaada kwa majirani wengine
ambao walifika hapo tukaanza jitihada ya kuwanasua ndani,”– Mwakasita.
Mwakasita amesema almkuta marehemu Mpira akiwa amesimama dirishani akisali.
“Alikuwa akisema Yesu wangu, Yesu wangu, lakini sikuweza kumuokoa kwa sababu moto ulikuwa tayari umetanda eneo kubwa la nyumba,”– Mwakasita.
Mmoja anusurika
Yusuph Lima amesema katika tukio hilo, Emmanuel Mpira ambaye ni baba wa watoto wawili waliofariki, alinusurika kutokana na wakati wa tukio alikuwa amelala nje ya nyumba hiyo kutokana na kulalamika joto, kwa sasa yupo hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiendelea na matibabu ya maradhi yake pamoja na mshtuko.
Yusuph Lima amesema katika tukio hilo, Emmanuel Mpira ambaye ni baba wa watoto wawili waliofariki, alinusurika kutokana na wakati wa tukio alikuwa amelala nje ya nyumba hiyo kutokana na kulalamika joto, kwa sasa yupo hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiendelea na matibabu ya maradhi yake pamoja na mshtuko.
Mwakasita walikuta maiti za watu hao zikiwa zimelala pamoja kwenye vyumba vitatu tofauti.
Waziri Mwandosya ni miongoni mwa viongozi waliofika eneo hilo kushuhudia tukio hilo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Wananchi wa eneo hilo wamelalamikia kikosi cha zimamoto kwa kitendo cha kuchelewa licha ya kupewa taarifa mapema.
Kamanda wa Polisi Ilala, Mary Nzuki amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo.
NIPASHE
Baadhi ya viongozi wa taasisi
zinazotuhumiwa kuwa vinara wala rushwa wameshangazwa na ripoti ya
utafiti wa AFROBAROMETER na kuhoji vigezo vilivyotumika.
Juzi AFROBAROMETER wakitangaza utafiti wao huku wakitaja taasisi hizo
na asilimia zake kwenye mabano kuwa ni Polisi (50), Mamlaka ya Mapato
TRA (37), Majaji na Mahakimu (36), TAKUKURU (29), Maofisa wa serikali
za mitaa (25), Watumishi wa Umma (25), Wabunge (22) na Rais na Maofisa
wa Ikulu (14).
IGP Ernest Mangu
amesema kuwa bado hajaipata ripoti ya utafiti huo na kuahidi pindi
utakapomfikia atazungumzia japo amesema hawajajua ni vitu gani
vilivyobainishwa kwenye utafiti huo na kuifanya Polisi kuwa kinara.
“Tukiupata tutauzungumzia kwani mpaka wamefikia maamuzi haya inawezekana kuna vitu wameviona na sisi hatuvijui,” IGP Mangu.Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah alisema kuwa hayupo tayari kujiingiza katika malumbano yoyote na kwamba yaliyosemwa dhidi ya taasisi yake hayamuumizi kichwa kwa kuwa anajua anachokifanya.
“Katika
kundi la watu hawakosekani wabaya wapo ambao hawatafanya vizuri hakuna
aliye malaika hata unapokuwa na watoto siyo wote watafanana kwa tabia,” Dk. Hoseah.
Dk. Hoseah ametahadharisha kuwa ifike pahala nchi iheshimike na siyo kila wakati ionekane kuwa ni chafu ama haina maana.
Mkurugenzi wa Elimu TRA, Richard Kayombo amesema
utafiti huo haujawafikia zaidi ya kuusikia kwenye vyombo vya habari,
huku akisema kuwa kwa upande wa TRA wana idara ya maadili ambayo
inafuatilia masuala ya tuhuma pale zinapotajwa na hatua kuchukuliwa,
wakiipata ripoti hiyo wataifanyia kazi.Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alipohojiwa kuhusu wabunge kutajwa katika ripoti hiyo amesema ni vigumu kujua kwa haraka na inawezekana mazingira hayo kuwapo, kama wabunge wametajwa itabidi wakutane na watafiti hao ili wawaeleze jinsi wabunge wanavyoingia katika rushwa .
MWANANCHI
Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani
kipo katika hatua za mwisho kuanzisha mfumo wa kulipa faini zote za
makosa ya barabarani kupitia benki na mitandao ya simu za mkononi ili
kupunguza malalamiko ya wananchi kuhusu vitendo vya rushwa na vitabu
bandia vya faini vinavyotumiwa na baadhi ya askari hao.
“Nina
uhakika na ninachokisema mpaka Julai mfumo huu utaanza kutumika,
tunataka kuboresha mfumo wa ulipaji faini na kuondokana na mianya ya
rushwa inayofanywa na baadhi ya askari wetu kama inavyolalamikiwa na
wananchi,” alisema Kamanda Mpinga.
Kamanda Mpinga amesema
mfumo huo ulitakiwa kuanza kazi mwaka jana ulishindikana kutokana na
ukosefu wa fedha za kununulia vifaa na maandalizi kwa ujumla.
MTANZANIA
Ikiwa imebaki kipindi cha mwezi mmoja kabla ya kuanza zoezi la kuchukua fomu za kugombea Urais, Ubunge na Udiwani, Waziri John Pombe Magufuli naye ametajwa kushawishiwa kuchukua fomu ya kugombea Urais huku akihakikishiwa kuungwa mkono na viongozi wa juu wa CCM.
Magufuli hakuwa na
mpango wa kugombea nafasi hiyo lakini inasemekana kuwa amepata ushawishi
huo kutoka kwa wakubwa hao ambaolengo lao ni kumzuia Edward Lowassa.
Rekodi nzuri ya utendaji wa Magufuli inatajwakuwa na nguvu kubwa ya kumkaribia Lowassa tofauti na wengine.
Mtu mmoja wa ndani kutoka makao makuu ya chama hicho Dar ameongea na gazeti la MTANZANIA
kwamba mwanasiasa huyo ameanza kujipanga baada ya kuhakikishiwa kuwa
jina lake litapitishwa katika vikao vya uteuzi ndani ya chama.
Nape Nnauye alikaririwa
kuwa uteuzi utakaofanywa na vikao vya chama hicho kumpitisha mgombea
wake wa Urais utazingatia umakini wa hali ya juu na kuwataka Watanzania
kujiandaa kwa kile alichokiita mshangao.
MWANANCHI
Mwanamke mmoja Sophia Nyabohe wa Serengeti mkoa wa Mara amekutwa amefariki kwa kujinyonga siku mbili baada ya kukamatwa kwa ugoni na mumewe nyumbani kwake.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Emmanuel Baro amesema baada ya kufumaniwa mwanamke huyo alikimbia kusikojulikana na baadaye kukutwa amejinyonga ndani ya chumba chao.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema baada
ya tukio hilo mume wa mwanamke huyo hakumsemesha wala kumuuliza kitu,
akawa hali chakula chake wala kuingia ndani ya nyumba hiyo ambapo
wanahisi kitendo hicho kilimzidishia mawazo mwanamke huyo akaamua
kujinyonga ili kuikwepa aibu hiyo.
Jeshi la Polisi limekirikupokea taarifa hiyo, kwa sasa wanaendelea na uchunguzi.
Nitaendelea kukusogezea kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment