Mkusanyiko wa Stori kubwa zilizopewa headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania February 16, 2015
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameitaka Serikali kuacha siasa kwenye masuala ya kiuchumi, ukiwamo mgogoro kati ya Tanzania na Kenya kuhusu sekta ta utalii.
Akifungua kikao cha Baraza la Uongozi wa
Chadema Kanda ya Kaskazini, Arusha jana, Mbowe aliwataka viongozi
Serikali kutumia busara kushughulikia mgogoro huo ulioibuka baada ya
Kenya kuzuia magari yenye usajili wa Tanzania kufika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
“Asilimia
40 ya watalii zaidi ya milioni moja wanaokuja Tanzania kila mwaka,
hupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta,”
“Hatustahili
kugombana nao, bali tunapaswa kutafuta namna bora ya kushirikiana.
Tuna uwezo wa kuchagua marafiki, lakini kamwe hatuwezi kuchagua
majirani. Hawa (Kenya) ni wenzetu, tutaendelea kuwa nao pamoja maisha
yote.
“Tutunge
sera nzuri ya usafiri wa anga na kuvutia kampuni kubwa za ndege kuja
kuwekeza nchini kwa kutumia viwanja vyetu, Kilimanjaro, Zanzibar, Dar es
Salaam na Mbeya:-Mbowe
Kuhusu sera na mfumo mpya wa elimu
uliozinduliwa juzi na Rais Jakaya Kikwete, Mbowe alisema tatizo la sekta
ya elimu siyo sera, bali bajeti finyu na usimamizi mbovu.
MWANANCHI
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe ameiomba Serikali ya China kusaidia kuimarisha ufanisi wa mamlaka ya Reli ya Tanzania TAZARA.
Membe alisema anafanya mpango wa kukutana na Rais wa Zambia na kuandaa mapendekezo watakayoyawasilisha kwa Serikali ya China.
Alisema reli ya Tazara ni eneo
linalotumika kwa kiasi kikubwa kuunganisha Mataifa hayo kiuchumi kwani
Zambia haina bandari na hutumia reli hiyo kusafirisha bidhaa kutoka Dar
es salaam kwenda Zambia.
Akizungumzia ukaribu wa Tanzania na
China Membe alisema nchi hizi ni marafiki katika Nyanja mbalimbali na
anaamini kuwa uhusiano huo utadumishwa kwa maendeleo ya Mataifa yote
mawili.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameitaka Serikali kuacha siasa kwenye masuala ya kiuchumi, ukiwamo mgogoro kati ya Tanzania na Kenya kuhusu sekta ta utalii.
Akifungua kikao cha Baraza la Uongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini,
Arusha jana, Mbowe aliwataka viongozi Serikali kutumia busara
kushughulikia mgogoro huo ulioibuka baada ya Kenya kuzuia magari yenye
usajili wa Tanzania kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo
Kenyatta.
“Asilimia 40 ya watalii zaidi ya
milioni moja wanaokuja Tanzania kila mwaka, hupitia Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta,”
“Hatustahili kugombana nao, bali
tunapaswa kutafuta namna bora ya kushirikiana. Tuna uwezo wa kuchagua
marafiki, lakini kamwe hatuwezi kuchagua majirani. Hawa (Kenya) ni
wenzetu, tutaendelea kuwa nao pamoja maisha yote.
“Tutunge sera nzuri ya usafiri wa
anga na kuvutia kampuni kubwa za ndege kuja kuwekeza nchini kwa kutumia
viwanja vyetu, Kilimanjaro, Zanzibar, Dar es Salaam na Mbeya,:-Mbowe.
Kuhusu sera na mfumo mpya wa elimu
uliozinduliwa juzi na Rais Jakaya Kikwete, Mbowe alisema tatizo la sekta
ya elimu siyo sera, bali bajeti finyu na usimamizi mbovu.
NIPASHE
Chama cha Wananchi (CUF),
kimepuliza kipenga kwa wanachama wake kikiwataka wajitokeze kuchukua
fomu za kugombea uongozi katika nafasi za udiwani, ubunge, uwakilishi na
urais unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kadhalika, chama hicho kimeweka
hadharani ratiba ya uchukuaji fomu, kura ya maoni, vikao vya kuchuja
majina ya wagombea wenye sifa na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la
Taifa kwa ajili ya kufanya uteuzi wa wagombea uwakilishi, ubunge na
urais.
Hata hivyo, ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu kwa nafasi ya urais kiporo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, jana jijini Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Shewaji Mketo,
alisema nafasi hizo zipo wazi kwa wanachama wote wenye sifa wanaotimiza
masharti ya Katiba ya nchi na chama kwa ajili ya kuwatumikia
Watanzania.
“Chama
kinatangaza kuwa kutakuwa na zoezi la kura za maoni kwa ajili ya
kuwapata wagombea wa udiwani, ubunge, uwakilishi na urais…uchaguzi huu
utafanyika ili kukidhi matakwa ya Katiba ya chama Ibara ya 91,92 na 93
pamoja na marekebisho yake”:-Mketo.
Mketo alisema pamoja na chama hicho
kuweka ratiba, malengo yao kama Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) yapo
pale pale na kwamba kila chama kitatafuta wagombea katika ngazi zote na
baadaye kuchambuliwa na vyama vya Ukawa ili kuona nani anastahili
kupewa wapi ya kuwa mwakilishi wa Ukawa.
Vyama vinavyounda Ukawa ni CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na NLD.
HABARILEO
Kutokana na wahalifu waliopambana juzi na polisi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kutokamatwa, hali ya wasiwasi imeendelea miongoni mwa wakazi wa mjini hapa.
Sasa wananchi hao wameiomba Polisi kutoa
tamko, kuhusu kikundi kilichorushiana risasi na askari Polisi na
kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja.
Aidha, wananchi hao wameitaka Polisi
kutoa ufafanuzi kuhusu mwendelezo wa matukio mengi ya uhalifu wa kutumia
silaha, ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi, ikiwemo kutokamatwa kwa
watuhumiwa wa matukio hayo.
Hata hivyo, Msemaji wa Polisi, Advera,
alisema Jeshi lake halina taarifa zaidi ya iliyotolewa juzi na Mkuu wa
Opersheni wa jeshi hilo, Kamishna Paul Chagonja.
Habari za kipolisi zinasema kwamba bado
wanaendelea kusaka wahalifu hao huku baadhi ya vikosi vya ulinzi na
usalama, vimeongezwa kwa ajili ya kupambana na wahalifu hao. Juzi Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi walipambana na kundi la
wahalifu katika maeneo ya mapango ya Amboni na kusababisha wanajeshi
wanne na polisi wawili kujeruhiwa.
Hata hivyo, kuna habari kuwa majeruhi
mmoja ambaye ni mwanajeshi alifariki baadaye akiwa hospitalini. Habari
zingine zinasema kwamba majeruhi wengine ambao ni polisi wanne na
mwanajeshi mmoja, wanaendelea vizuri. Kuhusu mwanajeshi aliyekufa,
polisi wamegoma kuzungumzia suala hilo, lakini habar
MTANZANIA
Wakati vita ya kuwania nafasi ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete
ikipamba moto, baadhi ya wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Kanda ya Ziwa, wamemtaka Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa,
agombee urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Wananchi hao katika kutimiza dhamira yao, wamemtuma Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa, Dk. Raphael Chegeni, kwenda kumshawishi Lowassa ili awanie nafasi hiyo.
Mjumbe huyo wa NEC ya CCM, Wilaya ya
Busega, alisema Lowassa anafaa kuwa rais hivyo atakwenda kumshawishi na
atamchangia fedha za kuchukulia fomu ya kugombea kwa kushirikiana na
marafiki zake ndani na nje ya CCM.
“Kati
ya waliojitangaza kutaka wapitishwe na CCM kumrithi Kikwete, bado
hatujaona mwenye sifa zinazotakiwa, sasa Dk. Chegeni kwa ushawishi wake
tunamtuma akamwambie Lowassa akubaliane na matakwa yetu, achukue fomu ya
kuwania urais kwani ndiye suluhisho la kero na changamoto za maisha ya
Watanzania,” alisema mmoja wa makada hao kutoka mkoani Kagera kwa niaba ya wenzake.
Alisema kwamba, Lowassa amekuwa kimya
muda wote licha ya kutajwa kwenye kinyang’anyiro hicho, lakini
atamshawishi agombee nafasi hiyo kwa kuwa anaamini ana uwezo wa
kuwatumikia Watanzania kutokana na rekodi yake ya utumishi wa umma
alipokuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya nne.
DIRA YA MTANZANIA
Wakati Serikali ikihaha kutafuta
mwarobaini wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika Mikoa ya
kanda ya Ziwa,katika hali isiyokuwa ya kawaida imebainika watoto ambao
huzaliwa wakiwa wamekufa huuzwa kwa waganga wa kienyeji.
Imedaiwa kuwa watoto hao huwa hawazikwi
kama livo kawaida na taratibu za hospitali,badala yake wauguzi wa
hospitali huwapeleka kwa waganga.
Tuhuma hizo zilitokea mbele ya Katibu tawala, Mwamvua Jilumbi katika kikao na wadau wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kukomesha vifo vya wajawazito na watoto Mkoani humo.
Wadau hao walieza kuwa viungo hivyo vimekuwa vikiuzwa kati ya 500,000 kiasi ambacho walieleza hutolewa na waganga hao.
JAMBOLEO
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mohamed Mpinga
amesisitiza kuwa ni marufuku magari binafsi kuweka tinted kwenye vioo
vya mbele kwa kuwa inakua vigumu kwa askari wa usalama barabarani
kutambua aliyeko ndani ya gari.
Alisema kuwa madereva wengine wanakata
sehemu ndogo kwa ajili ya kuangalia kioo cha pembeni na kama wanaweza
kukata sehemu hiyo kwa nini washindwe kuacha sehemu ya mbele ili kuona
vizuri.
“Gari
inapikuwa na tinted inakuwa ngumu kutambua kwa urahisi nani yupo,na
madhara yake hata kukiwa na majambazi huwezi kujua kwa urahisi..ni
marufuku vioo vya mbele kuwa na tinted“:-Kamanda Mpinga
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment