Friday, February 13, 2015

WAANDISHI WA HABARI EGPTY WAACHIWA HURU

Hii ni ya wale waandishi wa habari waliokamatwa Egypt…

077364-bb4c1454-456e-11e4-a4cb-76fb973361fc
Miezi 14 imepita tangu itolewe hukumu ya kifungo cha miaka saba kwa waandishi wa habari wawili na mwingine mmoja kufungwa miaka 10 kwa kosa la kuripoti habari za kichochezi wakiwa ndani ya Egypt wakati wa machafuko ya kisiasa, leo kuna taarifa nzuri kuhusu waandishi hao.
Mahakama ya Misri iliagiza kuachiliwa kwa waandishi wa habari wawili wa kituo cha Aljazeera, Baher Mohamed na Mohamed Fahmy waliohukumiwa kwa kosa la kuandika habari za kutetea kundi la Muslim Brotherhood ambacho baadaye kilipigwa marufuku kwenye nchi hiyo.
Mohammed Fahmy na Baher Mohammed wamekaa jela kwa zaidi ya siku 400 kila mmoja na mwenzao raia wa Australia, Peter Greste alirudishwa nyumbani kwao Australia kwa amri ya Rais Fattah el-Sisi, maamuzi ya Jaji wa Mahakama iliyotoa kibali cha kuachiliwa waandishi hao yanawaweka huru mpaka siku ya February 23 kwa ajili ya kusilizwa upya kwa kesi hiyo.
Davido CoversIII
Mohamed Fahmy (mwenye miwani akiwa ndani ya Mahakama)
Ndugu na jamaa wa waandishi hao waliokuwa Mahakamani hapo walipokea kwa furaha taarifa za ndugu zao kuachiwa, huku masikio na macho yao wakisubiri hukumu itakatotolewa kwa mara ya pili.
Waandishi  wengi duniani walilaumu kitendo cha kufungwa Wanahabari hawa wakidai kuwa ‘wamefungwa kwa hatia ya kutekeleza majukumu yao’.
Mohammed Fahmy, mwandishi wa Habari wa Al Jazeera
Mohamed Fahmy, mwandishi wa Habari wa Al Jazeera ambaye ni raia wa Canada.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment