Tangakumekuchablog
Tanga, WACHIMBAJI wa mawe na kokoto eneo
ambalo limetokea machafuko ya kujibizana risasi baina ya polisi kwa
kushirikiana na jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wamevitaka vyombo vya usalama
kulimaziza tatizo hilo ili familia zao zisiteseke.
Wakizungumza
na tangakumekuchablog kijiji
cha Mleni nje kidogo ya Amboni, wachimbaji hao wamesema hadi sasa hawajui namna
gani wataweza kuziendesha familia zao kutokana na vyombo vya usalama kuwazuia
kuingia eneo la machimbo.
Walisema
maisha yao wamekuwa wakiyaendesha kulingana na kazi wanazozifanya machimboni
huko na hivyo kuwataka kulimaliza sekeseke hilo ambalo wanahofu ya kuchukua
muda mrefu.
“Leo hapa
sisi tupo siku ya pili tumejikalia na kulala kama unavyotuona hatujui tufanye
nini-------familia zetu tumezipeleka mjini zisije kufa kwa njaa” alisema
Emmanuel Keshi
“Sisi hapa
tunashindia maji na wasamaria wema kutugaia mikate na kuweza kuuwa njaa----ila
jamii itambue kuwa tuko katika mzingira magumu kwani tukio hili limekuja bila
taarifa” alisema
Kwa upande
wake mchimbaji wa kokoto na mawe, Ossea Nyenga, alisema katika eneo hilo la
mapango na machimbo wamekuwa wakifika watu kila aina na kutojua mwema na mhalifu
ni yupi na kushauri ni vyema kuweko
sheria .
Alisema
eneo hilo la mapngo ni kubwa na watu kuingia na kutoka bila kuwa na
kitambulisho na hivyo kushauri yoyote ambaye atakuwa anaingia kuwa na kibali au
kitambulisho wakiwemo watalii.
“ Hili
eneo la mapango ni la kitalii lakini tunashindwa kuiona Serikali yetu ikiliweka
kama sehemu ya kitalii au hifadhi ya taifa-----watu wa kila aina wanakuja
kutalii wengine wamo wenye dhamira mbaya” alisema Nyenga
Amevitaka
vyombo vya usalama kulimaliza tukio hilo ambalo limetetemesha Tanga na nje na kama kuna dalili zozote za kihalifu kuweza
kuchuliwa hatua ili hali za wananchi kurejea na kufanya kazi zao kwa amani.
|
Sunday, February 15, 2015
WAHANGA WA SEKESEKE LA AMBAONI TANGA WALIA NJAA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment