Umeipata hii ya mapacha watatu Kenya kufaulu kwa matokeo sawasawa?
Mapacha hao Abenego Bingi, Meshak Barongo na Shadrack Isangoma
walipata alama ya B- ambazo ni 55, 56 na 57, wamesema wanapenda sana
somo la kiswahili ambalo walifanya vizuri kwenye mtihani huo wa kitaifa.
Mama yao Bi Eugene Amoti
ambaye ni Mchungaji katika Kanisa la New Light Kisumu, anasema kuwa
mapacha hao walikuwa na viwango tofauti vya kufaulu kwa masomo yao, kila
wakati walikuwa wakipata alama tofauti.
Story hii kwenye ukurasa wa gazeti la ‘Taifa Leo’, Kenya.
Walimu wa Shule ya Kisumu Day wamesema wameshangazwa sana matokeo hayo ambayo wanayaona kama baraka kwa shule hiyo.
No comments:
Post a Comment