Mchungaji kashtukia usaliti unaofanywa na mchungaji mwenzake kwa mkewe..
Nina hii stori kutoka Nigeria, Mchungaji
mmoja kaamua kumuandikia mke wake talaka kutokana na kugundua kuwa mke huyo ana uhusiano na mchungaji mwenzake ambaye ni rafiki yake wa karibu
pia.
Mchungaji Jack aliiambia Mahakama ya Lagos, Nigeria kwamba aligundua uhusiano wa mkewe Kate na mchungaji huyo baada ya kuhama nyumba ambayo walikuwa wakiishi wote tangu mwaka 2011 na hajawahi kurudi tena.
Hata hivyo Kate
hakuhudhuria Mahakamani hapo, kuna ripoti zinazosema kwamba mwanamke
huyo amefanya kama kususia kuhudhuria kesi hiyo Mahakamani ambapo
Mahakama imetoa amri aandikiwe barua ya kuitwa tena kwenye kesi
itakayosikilizwa March 23.
Hakuna Stori itakayokupita ,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment