Taarifa nyingine kutoka Iringa kuhusu ajali ya basi iliyotokea juzi MARCH 11
Idadi ya watu waliofariki katika ajali
ya basi la Majinja lililogongana na lori siku ya jana Mkoa wa Iringa
imeongezeka na kufikia watu 50.
Idadi hiyo ya watu imetokana na Uongozi
wa Mkoa wa Iringa kupitia upya idadi ya maiti waliotokana na ajali hiyo
pamoja na mgonjwa mmoja kufariki baada ya kufikishwa Hospitali.
Mkuu wa Mkoa Iringa amesema chanzo cha ajali hiyo sio ubovu wa barabara pekeyake; “sio barabara pekee iliyopelekea ile ajali.. spidi, ufinyu, mtelemko.. hakuna alama. Nimemuagiza Manager
wa TANROADS jinsi yoyote ile atakavyofanya.. lakini pia tumepata mdau
ametusaidia mafuta ambayo yatamsaidia pia meneja wa TANROADS eneo hilo
linahitaji fedha za matengenezo ya dharura…”– Amina Masenza, Mkuu wa Mkoa Iringa.
No comments:
Post a Comment