Twitter yapitisha utaratibu huu mpya kwa watumiaji wake.
Mtandao wa Twitter umebadili sheria zake katika kuzuia watumiaji wake kuchapisha Picha na video chafu.
Sheria ya mtandao huu wa kijamii inasema ni ”Marufuku
kuchapisha picha au video chafu zilizopigwa au kurekodiwa kisha
kusambazwa bila ridhaa ya muhusika aliye kwenye video na picha hizo”
Mwezi uliopita vitendo hivi vilitambulika kuwa makosa ya jinai nchini Uingereza na Wales.
Msemaji wa Kampuni ya Twitter amesema watumiaji watakaobainika kukiuka masharti mapya akaunti zao zitafungiwa.
Watumiaji wanaopeleka malalamishi
Twitter kuhusu picha na Video zilizochapishwa watatakiwa kujitambulisha
na kuithibitishia Kampuni kuwa hawakuwahi kutoa idhini ili kuchapisha
picha au video mtandaoni na kuonekana hadharani.
Nchini Uingereza na Wales imeweka sheria ambayo mtuhumiwa atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka miwili gerezani.
Sheria hiyo inagusa picha zinazowekwa
kwenye mitandao ya kijamii na Ujumbe mfupi huku majimbo kadhaa ya
Marekani yameweka Sheria ya kupambana na vitendo hivi hasa California,Texas na Utah.
Hakuna Stori itakayokupita ,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment