Pamoja na kushinda ubingwa wa dunia, bondia Cosmas
Cheka amerejea nchini bila ya mkanda.
Bondia huyo ambaye ni mdogo wake na bingwa mwingine wa
Francis Cheka amerejea nchini bila ya mkanda huo.
Cheka amemtwanga bondia wa Thailand na kutwaa ubingwa
wa uzito mwepesi wa WBO, lakini wenyeji wakaamua kutompa mkanda.
Taarifa zinaeleza, promota alionekana kukerwa na Cheka
kumpiga bondia wao hadi kufikia uamuzi wa kumnyima.
Lakini juhudi zimekuwa zikifanyika kuwasiliana na WBO
kuhakikisha mkanda huo unatumwa nchini.
No comments:
Post a Comment