Ikitokea Jose Mourihno kafukuzwa Chelsea, hiki ndio kiwango cha pesa atakacholipwa…
Mabingwa wa ligi kuu England Chelsea
imepata matokeo mabaya mfululizo na kusababisha kuwa na sintofahamu juu
ya kibarua cha kocha wao Jose Mourinho.
Pamoja na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich kukanusha
kumtimua kocha huyo lakini ukweli ni kwamba endapo watadhubutu kufanya
hivyo itawalazimu kumlipa Kocha huyo kwa kumlipa kiasi cha Euro milioni
30.
Mourinho
aliongezewa mkataba mwingine wa mwaka mmoja usiopungua Euro milioni 8.5
na kumfanya kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo hadi mwaka 2019.
Kutokana na matokeo mabaya wanayoyapata
kwa sasa mabingwa hao watetezi wapo katika hatari ya kuukosa uchampion
wa ligi hiyo msimu ujao.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment