Thursday, October 15, 2015

HELKOPTA YAANGUKA NA KULIPUKA

Helikopta imeanguka na kulipuka… Waziri amtaja Mbunge wa CCM aliyekuwemo.

Usiku wa October 15 2015 zinatoka taarifa kupitia Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu kuhusu ajali ya helikopta iliyotokea kwenye mbuga ya wanyama ya Selous ikiaminika kuwa na Wanasiasa ndani yake.
Taarifa aliyoitoa imeeleza hivi >>> ‘Tumetuma vikosi vya maafisa na maaskari katika eneo la Selous kulikotokea ajali ya helikopta katika harakati za uokozi, ajali ya helikopta imetokea katika kitalu R3 ndani ya mbuga ya Selous na mashuhuda wanasema ilianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha
Mashuhuda wa ajali ya helikopta iliyotokea Selous walikuwa kitalu R2 na walishuhudia ikianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha Kitalu R3, Maafisa na Maaskari wanaelekea eneo la tukio kutokea Msolwa na Matambwe na tumeagiza vikosi vilivyo kwenye doria Selous kushiriki uokoaji
Deo
Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa (CCM)
Mashuhuda wa ajali ya helikopta Selous walikuwa Kitalu R2 wanasema ilianguka baada ya majira ya saa 12 jioni na kulipuka, serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii inachukua hatua zote kuwafikia wahanga na majeruhi wa ajali ya helikopta Selous usiku huu
Nimeagiza section 2 zenye askari 16 kutoka Matambwe na Msolwa (Selous) kwenda eneo la tukio, RPC Morogoro na mkuu kanda ya Msolwa (Selous) wanashirikiana, hatujui kitakachokuwa kimewapata wasafiri ndani ya helikopta iliyoanguka akiwepo Mh, Filikunjombe, tuungane kuwaombea kwa Mungu <<< Lazaro Nyalandu
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment