Tangakumekuchablog
Tanga,MGOMBEA
Udiwani kata ya Mnyanjani kwa tiketi ya ACT, Wazalendo, Suleiman Khafidh haachi
vituko vyake na mara hii amesema endapo atachaguliwa kuwa Diwani nyumba zote za
makuti zilizoko ndani ya kata yake ataziweka bati moja baada ya nyengine kwa kutumia mshahara wake.
Mgombea huyo kijana machachari
ameyasema hayo juzi uwanja wa mabatini na
amekuwa kivutio kila apandapo jukwaani kwani haachi kutoa vituko jambo
ambalo limekuwa likiwavutia watu wengi.
Alisema anatambua kuwa hakuna mtu
anaependa kuishi katika nyumba ya makuti lakini ni kutokana na umasikini na
hivyo kusema kuwa wakimchagua mshahara wake wa kila mwezi atakuwa akinunua
bati na kutoa nyumba mmoja baada ya nyengine.
“Ndugu zangu wananchi napatwa na
uchungu kuona wazee wangu na ndugu zangu wakiishi katika nyumba za
makuti----natambua kuwa hakuna anaependa hali hii hivyo nichagueni niwaekeeni
bati kupitia pesa za mshahara wangu” alisema Khafidh na kuongeza
“Nikishuka katika jukwaa hili nitaanza kuzihesabu nyumba mmoja mmoja ili
kupata idadi kamili ---lengo nikupata tathmini ili mshahara wangu nikipokea tu
nakimbilia dukani” alisema
Mgombea huyo wa Udiwani aliwataka
wananchi wa kata hiyo kutofanya makosa kwa kumchagua diwani mwengine kwa madai
kuwa yeye yuko na uwezo wa kuibadilisha kata hiyo na kuwa kama posta Dar es
Salaam/
Alisema kitu ambacho atakipa kipaumbele
mara baada ya kuutwaa Udiwani ni kuhakikisha anaweka miundombinu ya kutiririsha
maji kuelekea baharini pamoja na kumwaga kifusi katika mabwawa ili kumaliza mazalia ya mbu na malaria.
Alisema kata hiyo iko na kero ya
mazalia ya mbu wakati wa mvua kunyehs kutokana na maji hayo kutokuwa na njia ya
kupitisha na hivyo kutoa ahadi ya kulimaliza kero hiyo.
“Vipaumbele vyangu nikiwa ni diwani
wenu kwanza nitachimba mfereji wa kupitisha maji ya mvua na majumbani yaelekee
baharini----vipindi vya mvua hapa kwetu ni sawa na ziwa Victoria” alisema
Suleiman
Alisema ili kuweza kuja maendeleo ya
kweli ni kuhakikisha kura zote za udiwani zinakuja kwake pamoja na
kumpigia mgombea Rais wa chama chake ili
kuweza kuwabadilishia katika mfumo wa maisha
duni wa sasa .
Mwisho
No comments:
Post a Comment