Matokeo ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Euro 2016 yapo hapa.
Michuano ya kuwania kufuzu kucheza Euro 2016
imeendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali, moja
kati ya mechi zilizochezwa usiku wa October 9, timu ya taifa ya Uingereza ilikuwa mwenyeji wa timu ya taifa ya Estonia.
Mechi ambayo ilikuwa ngumu kwa Uingereza kuweza kupata nafasi ya kufunga goli kutokana na timu ya taifa ya Estonia
kuwa imejiandaa vyema kuwakabili waingereza hao, uwezo wa kuhimiri
mashambulizi ya waingereza ulidumu kwa dakika 44 kabla ya dakika ya 45 Theo Walcott kupachika goli la kwanza na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0 dhidi ya Estonia.
Uingereza walirudi uwanjani kipindi cha pili wakiwa na faida ya goli moja kitu ambacho kiliwapelekea Estonia kujaribu kutafuta nafasi ya kusawazisha goli hilo ila Raheem Sterling aliwakatisha tamaa ya kusawazisha goli hilo ambalo lingeweza kuwafanya waondoke na Point moja, Sterling alipachika goli la pili dakika ya 85 ya mchezo na kufanya mechi imalizike kwa Uingereza kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Matokeo ya mechi nyingine za kuwania Euro 2016 zilizochezwa usiku wa October 9
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment