Thursday, October 8, 2015

KUFURIKA KWA MAGEREZA MAREKANI, KICHEKO KWA WAFUNGWA

Magereza yamejaa Marekani.. Hawa ndio wafungwa ambao imebidi waachiwe huru..!!


Idara inayohusika na Masuala ya Sheria Marekani iko kwenye mpango wa kurekebisha Sheria pamoja na kuwaachia huru wafungwa 6,000 baada ya Magereza mengi ya nchi hiyo kuonekana yamefurika Wafungwa kwa sasa !!
Moja ya sababu ambazo zimetajwa kuchangia Magereza mengi kujaa ni ishu ya Sheria kali zilizowekwa Marekani kwa Watuhumiwa wa Kesi za dawa za kulevya.
Kwenye idadi hiyo ya Wafungwa watakaoachiwa wengi wao ni wenye Kesi za Dawa za Kulevya na hata kabla ya kuachiwa pia kuna vitu vingi vitaangaliwa kuhusu usalama wa maisha ya watu wengine nje baada ya Watuhumiwa hao kuachiwa.
Wafungwa hao wataanza kuachiwa kuanzia October 30 mpaka November 02 2015… Mpaka mwisho wa mwaka 2014 Takwimu zinaonesha kulikuwa na Jumla ya Wafungwa Milioni 1.56 kwenye Magereza ya Marekani, huku Takwimu nyingine zikionesha Marekani ina Magereza mengi zaidi kuliko idadi ya Vyuo vilivyopo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment