Thursday, October 8, 2015

INDIA YATENGENEZA GARI KUBWA NA KUVUNJA REKODI

Raia wa India atengeneza gari kubwa duniani

Mchoraji wa miundo ya magari nchini India Sudhakr Yadav amejaribu kuweka rekodi ya pili ya Guiness kwa kutengeneza gari kubwa litakuwa ndilo kubwa zaidi duniani.
Gari hilo, ambalo limeundwa likifanana na gari aina ya Ford Toure lililoundwa mwaka 1922, lina urefu wa futi 26 (mita 8) kwenda juu na ukubwa wa futi 50 lina ukubwa maradufu wa basi lililo na ghorofa mbili mjini London.
 Yadav tayari anashikilia rekodi ya kitabu cha Guiness kwa kuwa na baiskeli ndefu zaidi duniani.
Mchoraji huyo wa miundo ya magari anamiliki makavazi ya magari katika mji wa Hyderabad ulioko kusini mwa India ambapo anaonyesha mitindo tofauti ya magari.

Anatarajia gari hilo liwe na mngurumo sawa na wa magari ya mbio za langalanga au Formula One.
Baiskeli yake ya magurudumu matatu ni ndefu zaidi ya gari hilo ikiwa na futi 41.5 kwenda juu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment