Thursday, October 1, 2015

LIVERPOOL YABANWA

Matokeo ya mechi ya Liverpool Vs FC Sion yapo hapa

Oktoba 1 mechi za UEFA Europa ziliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya, kama ambavyo imezoeleka kwa mechi za klabu Bingwa Ulaya huchezwa kati kati ya wiki siku ya Jumanne na Jumatano, UEFA Europa huchezwa siku ya Alhamisi.
_85865374_divockorigi
Alhamisi ya Oktoba 1 imepigwa michezo kadhaa ikiwemo mechi ya Liverpool ya Uingereza dhidi ya Sion ya Uswiss, mechi imepigwa katika uwanja wa Anfield ambao ndio uwanja wa nyumbani wa Liverpool. Mchezo ambao ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili, ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, Liverpool  walikuwa wa kwanza kuona nyavu za Sion kupitia kwa Adam Lallana dakika ya 5 ya mchezo.
_85865426_tv029400111
Sion ambao walikuwa wageni wa Liverpool katika dimba la Anfield walianza kuonesha jitihada za kutaka kusawazisha goli hilo dakika za mapema tu ila dakika ya 18 kipindi cha kwanza Ebenezer Assifuah alifanikiwa kusawazisha goli hilo baada ya kutumia vema krosi iliopigwa kutokea kati kati ya uwanja na kufanya mechi imalizike kwa jumla ya goli 1-1.
_85865430_tv029401713
_85865373_rexfeatures_5207504h


Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment