Thursday, October 1, 2015

MBWA AMZIDI AKILI MCHUNGA WAKE, AELEWA LUGHA KWA WIKI TATU TU

Mbwa atumia wiki tatu kujifunza lugha mpya

Ginger
Mbwa aliyekuwa akiandamana na mmiliki wake kwenye darasa la kujifundisha lugha ameshangaza wengi baada ya kuanza kuelewa lugha hiyo baada ya wiki tatu pekee.
Neil Smith alikuwa akiandamana na mbwa wake mwenye umri wa miaka mine kwa jina Ginger akienda kujifunza lugha ya Gaelic katika kanisa moja karibu na mji wa Dunoon.
Anasema alishangaa kuona jinsi mbwa huyo aina ya English Cocker Spaniel alianza kufuata maagizo yaliyotolewa kwa lugha hiyo kama vile keti (suidh), kaa (fuirich), njoo hapa (trobhad) na mbwa mzuri (cu math).
Mwalimu Elma McArthur alisema Ginger ni mbwa mwerevu sana.
 Smith na Ginger wamekuwa wakihudhuria darasa hilo katika kanisa la Strone Church of Scotland kila wiki pamoja na watu wengine 23.
Neil Smith
Mzee huyo wa miaka 67 alimsifu mbwa huyo wake anayemsaidia kusikia akisema imemuwezesha kujiamini zaidi.
Anasema sasa anafurahia kujionyesha kwa watu wengine na kujivunia kwamba ana mbwa anayefahamu lugha mbili.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment