Sunday, October 4, 2015

MKE WA LOWASSA APIGA HODI TANGA, AZANGUMZA NA WANAWAKE

  Mke wa mgombea Urais kupitia Chadema, Regina Lowassa, akingia ukumbini kuzungumza na wanawake jimbo la Tanga kuzungumza mambo mbali mbali yakiwemo ya kumpigia kura mume wake, Edward Lowassa uchaguzi mkuu October 25.


 Mke wa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Regina Lowassa, akiangalia zawadi aliyopewa na wanawake wa Tanga  (leo) wakati wa kikao na wanawake wa jimbo la Tanga.mjini ambapo maelfu ya wanawake walijitokeza na kumlaki mke wa mgomnea huyo wa Urais kupitia Ukawa. na kuzungumza mambo mbali kuelekea uchaguzi mkuu mwezi huu na kuwataka wanawake kujitokeza kwa wingi na kuitumiahaki yao kumpigia kura Lowassa na wagombea nafasi za Ukawa

Alisema endapo watamchagua Lowassa ataibadilisha nchi kutoka katika dimbwi la umasikini na kuhakikisha maisha ya kila mtu ikiwemo kuboresha huduma za kijamii ikiwemo hospitali pamoja na shuleni ambapo kila mtoto anaefikisha umri wa kwenda shule anapatiwa haki yake bure hadi chuo kikuu.
 Mke wa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Regina Lowassa, akitoka katika mkutano wa wanawake ulioitishwa na wanawake wa jimbo la Tanga mjini leo
  Mke wa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Regina Lowasa, akisalimiana na wanachama kupitia Ukawa Tanga  leo wakati wa mkutano ulioitishwa na wanawake wa jimbo la Tanga

No comments:

Post a Comment