Tangakumekuchablog
Tanga,MGOMBEA
Urais kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hshimu Rungwe, amesema endapo
Watanzania watamchagua kuwa Rais
atahakikisha anafufua viwanda na
bandari zilizokufa.
Akizungumza katika mkutano wa
kampeni leo uwanja wa Tangamano, Rungwe, alisema Tanga ulikuwa mji wa viwanda
na usafiri wa reli ambavyo vyote vimekufa jambo ambalo wananchi wake wamerudi
katika umasikini na watu kuukimbia.
Alisema uwezo wa kuurejesha mji wa
Tanga katika nafasi yake ya viwanda na usafirishaji wa shehena kwa kutumia
bandari yuko nao hivyo kuwataka wananchi kumpa kura kwa wingi na kuweza
kuongoza nchi.
“Mji wa Tanga ulikuwa unasifika
kuongoza kwa viwanda na hakuna ubishi hapa kulikuwa hakuna umasikini-----wageni
walikuwa wanamiminika na umasikini hapa haukuwepo” alisema Rungwe na kuongeza
“Musifanye kosa kuchagua kiongozi ambaye
hana uchungu na wananchi----natambua hapa vyote toka mumekunywa chai na andazi
moja au mawili asubuhi hamjala uwongo kweli” aliuliza
Akizungumzia bandari ya Tanga, Rugwe
alisema imeshindwa kufanya kazi kutokana na viongozi kung’ang’ani bandari ya
Dar es Salaam na kusababisha msongomano na foleni barabarani na kuwa usumbufu
kwa wananchi.
Alisema atahakikisha bandari hiyo
inafanya kazi kama ilivyo bandari ya Dar es Salaam kwa meli kubwa kushusha shehena na kuwavutia
wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.
Alisema hakuna sababu ya wafanyabiashara
wa Tanga kushusha mizigo yao bandari ya Dar es Salaam wakati Tanga ipo na kudai
kuwa hapo kuna ukiritimba ambao akiwa Rais atauondosha.
“Bandari yenu inakimbiwa na hata wafanyabiashara wa
hapahapa munajua kwanini----ni ukiritimba ambao mimi naujua hivyo nipeni kura
nyingi niwe kiongozi wenu muone Tanga itakavyopendeza” alisema Rungwe
Aliwataka vijana wazee na makundi
yote ya walemavu kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kumchagua yeye
kuwa Rais wao na kuondosha umasikini ambao kila siku umekuwa ukikua na
kuwaumiza wananchi.
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chaumma, Hashimu Rungwe akimtangaza mgombea Udiwani kata ya Mzizima wa Chama hicho, Bakari Hamis wakati wa mkutano wake wa kujinadi kupitia nafasi hiyo ya Urais uwanja wa Tangamano
No comments:
Post a Comment