Daktari wa zamani wa Chelsea ameshangazwa na maamuzi ya FA juu ya kesi yake na Jose Mourinho …
Kati kati ya mwezi September kulikuwa na stori kuwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho huenda akafungiwa na shirikisho la mpira wa miguu Uingereza FA kutokana na kitendo cha kumfanyia ubaguzi wa kijinsia aliyekuwa daktari wa timu ya Chelsea Eva Carneiro. Uchunguzi ulifanyika na kuwasilishwa katika shirikisho la soka Uingereza FA.
Stori baadae zilitoka kuwa mwenyekiti wa FA Greg Dyke alisema Mourinho anatakiwa kumuomba msamaha Eva Carneiro, October 2 Eva Carneiro amelilaumu shirikisho la mpira wa miguu Uingereza FA kwa sababu halikutaka kumuhoji chochote kuhusiana na suala hilo licha ya kuwa vielelezo viliwasilishwa FA.
“Nilishangazwa
kuona FA wanafanya uchunguzi wa tukio la August 8 katika mkutano na
waandishi wa habari, sikuwahi kuombwa na FA niandike maelezo kuhusiana
na tukio hilo sijui ndio mfumo rasmi wa uchunguzi katika nchi hii,
ambapo ushahidi wa wahusika hakuzingatiwa” >>> Eva Carneiro
Eva Carneiro aliingia katika malumbano na kocha wa Chelsea Jose Mourinho August 8 katika mechi dhidi ya Swansea City, mchezo ambao ulimalizika kwa sare, Jose Mourinho alimlaumu Eva Carneiro baada ya kuingia uwanjani kutoa huduma kwa Eden Hazard katika dakika za lala salama, hivyo Mourinho anaamini Eva Carneiro alichangia kuchelewesha muda.
Baada ya Eva Carneiro na msaidizi wake Jon Fearn kutoka uwanjani inasemekana Mourinho alimtolea lugha sio nzuri Eva Carneiro kwa kumuita “filha de puta” maana
yake ni kuwa binti wa mwanamke muhuni. Maana hii ilitolewa baada ya
uchunguzi kufanyika kwa kuwatumia watafsiri wa lugha ya kireno.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment