Monday, October 5, 2015

SWIMING POOL INAYOELEA, JE UMEWAHI KUONA"

Unapenda kuogelea? Karibu kwenye hii Swimming Pool inayoelea juujuu…

Hii ni katikati ya Jiji la London Uingereza… Kama wewe ni mpenzi wa kuogelea au kwenda zako swimming na watu wako, unaweza kucheki na hii swimming pool iliyokaa kwenye muundo wa tofauti kabisa !!
Tumezoea kuona swimming pool zilizojengwa kwenye ardhi, uliwahi kufikiria kwamba kuna mtu atafanya ubunifu wa swimming pool inayoelea juujuu ?!!
Pool IV
Kazi inafanywa kwenye apartments ambazo ziko kwenye Jengo la Ghorofa kumi, watu wataenjoy kuogelea juujuu, ujenzi unafanyika kwa kioo kitupu kwa hiyo unaambiwa unapoogelea unapata raha zaidi ya kujihisi kabisa kwamba unaogelea angani.
Wataalam waliokabidhiwa Ujenzi wamesema kazi itakamilika soon na mpaka 2018 kazi itakuwa imekamilika na wapangaji watakuwa wameanza maisha yao rasmi kabisa.
Pool III
Pool V
Unaweza kucheki kipande cha video hapa mtu wangu, jamaa wanasema kazi ikikamilika itakuwa ndio swimming pool ya kwanza inayoelea angani Duniani

No comments:

Post a Comment