TAARIFA MPYA KUTOKA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS,
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewateua wakuu wa wilaya wapya 13 na kuwahamisha vituo vya kazi wengine
saba.
Wakuu wa
wilaya 13 walioteuliwa ni Shaaban Athuman Ntanambe ambaye anakuwa Mkuu
wa Wilaya ya Chato, Mkoa wa Kagera; Thabisa Mwalapwa ambaye anakuwa Mkuu
wa Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara; Richard Kasesera ambaye anakuwa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Ruth Msafiri ambaye anakuwa
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma na Abdallah Njwayo ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Wakuu wa
Wilaya wengine wapya ni Asumpta Mshama ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya
Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe; Mohammed Mussa Utaly ambaye anakuwa Mkuu
wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma; Dauda Yasin ambaye anakuwa Mkuu wa
Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe; Honorata Chitanda ambaye anakuwa Mkuu
wa Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera; Vita Kawawa ambaye anakuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga na Christopher Ng’ubyagai ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida.
Wakuu
wengine wapya ni Hawa Ng’humbi ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu,
Mkoa wa Shinyanga na Mrisho Gambo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya
Uvinza, Mkoa wa Kigoma.
Wakuu wa
wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye anatoka
Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda Wilaya ya Arusha, Mkoa wa Arusha; Wilson
E Nkambaku ambaye anahamishiwa Arumeru, Mkoa wa Arusha kutoka Kishapu,
Mkoa wa Shinyanga; Francis Miti ambaye anahama Wilaya ya Hanang, Mkoa wa
Manyara kwenda Monduli, Mkoa wa Arusha na Jowika Kasunga ambaye
anahamia Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa kutoka Monduli .
Wengine
waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka Wilaya ya Makete, Mkoa wa
Njombe kwenda Wilaya ya Morogoro; Hadija Nyembo ambaye anahamia Wilaya
ya Kaliua, Mkoa wa Tabora kutoka Uvinza, Mkoa wa Kigoma na Benson
Mpyesya ambaye anahamia Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma kutoka Kahama.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment