Tangakumekuchablog
Tanga, MGOMBEA
Ubunge jimbo la Tanga mjini kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Mussa Mbarouk,
amesema mara hii hatokubali kuibiwa kura zake na atakae jaribu atakula ngumi
kali Kama za Mike Tyson.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara juzi, kata ya Marungu juzi, Mussa alisema upole wake utaisha pale
atakapobaini mtu kumuibia kura zake na tayari ameshanunua gloves za kuvaa
mikononi.
Kauli hiyo iliamsha shangwe na
vifiko kwa watu waliojazana uwanjani hapo na baadhi ya watu walimtaka mgombea
huyo kutenga muda wake wa kufanya mazoezi kwani kuna watu wamezoea kuiba kura.
“Ndugu zangu musinione mimi mpole mpole mukadhani ni legelege----mimi
nimeshapitia kila aina ya mazoezi yakiwemo ya kupigana mandonga ila
sijabahatika tu kubeba mkanda” alisema Mussa na kuongeza
“Nipelekeeni salamu zangu kwa waizi
wa kura na waambieni kuwa nimeshanunua gloves maalumu kwa kuwatwanga na ni
kali zaidi ya Mike Tyson” alisema
Mussa alisema Push up za CCM
haziwanyimi usingizi na kudai kuwa wamechelewa kwani wao sasa hivi
wanafanya mazoezi ya kupasha misuli
kusubiri kusherehekea ushindi wa kimbunga.
Alisema ukiwaangalia hao wapigaji
push up hawafikishi hata tano na kusema yoyote atakaefikisha kumi atampa mabata
wawili akafanye mboga nyumbani kwake.
Mussa alisema ushindi mwaka huu ni
mweupe kuanzia Udiwani, Ubunge hadi Urais hivyo kuwataka wananchi kuwapatia
kura nyingi wagombea wa Ukawa na kuwaonyesha CCM kuwa nchi hii sio masikini
ila kuna watu wanaowapa umasikini wananchi.
Akizungumza katika mkutano ambao
ulihudhuriwa na mgombea Udiwani wa Ngamiani Kati, Habib Mpa,(CUF) ,amedai mwaka
huu chama hicho kiko na uhakika wa kuongoza halmashauri na kula kuku kwa mrija.
Alisema kwa mahesabu ya harakahara
ni kuwa CUF itanyakua viti zaidi ya 20 hivyo kutaka kuwaonyesha wananchi kuwa
maendeleo yalikuwa yakikwamishwa na madiwani wa CCM.
“Ndugu zangu wa Marungu kazeni buti
na tumuombe Mungu isije tokea dharura mmoja wetu akakosa haki ya kupiga kura
kwani CCM wanatuombea mabaya ili kura zetu zipungue lakini nawaomba tuwageuzie
kibao iwe wao ili tule kuku kwa mrija” alisema Mpa
Mpa aliwataka wananchi wa kata ya
Marungu kutofanya kosa kwa kumchagua mgombea mwengine asiekuwa wa CUF kwa madai kuwa chama hicho kimechoka na hivyo
kutakiwa kupumzishwa .
Mwisho
No comments:
Post a Comment