Tangakumekuchablog
Tanga, KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya
Tanga, Lupassio Kapange, amemtaka mgombea Ubunge jimbo la Tanga, Omari Nundu
kupeleka posa kwa mgombea Ubunge jimbo la Tanga na mgombea Udiwani kata ya
Mwanzange wote kupitia CUF kwa madai kuwa hawana heshima.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni
wa kumnadi Nundu Leo, Kapange alisema kutokana na sheria ya dini ya dini ya
Kiislamu kuruhusu muumini kuoa wake wanne, hivyo mgombea huyo nafasi yuko nayo
hivyo kupelekea posa kwa mgombea wa Ubunge, Mussa Mbarouk na mgombea Udiwani
kata ya Mwanzange, Rashid Jumbe.
Alisema wagombea hao katika mikutano
wamekuwa wakitoa maneo yasiyofaa na ili kuweza kuleta heshima ni mgombea huyo
Omari Nundu kupeleka posa na kuweza kuwa shemeji yao.
“Hawa watu wamekuwa wakimsema vibaya
mgombea wetu kwani wanatambua kuwa hawawezi kushinda na ndio maana wanasema
sema hovyo hovyo----sasa nakuomba mheshimiwa peleka posa waweze kukuheshimu”
alisema Kapange na kuongeza
“Mheshimiwa najua wewe ni muislamu
safi na umeshawahi kwenda hijja na uko na mke mmoja---kwa vile dini yako
inakuruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja hebu peleka posa kwa Mussa Mbarouk na
Rashid Jumbe uwazibe midomo ya kusema sema” alisema
Akilijibu hilo jukwaani mara baada
ya kupewa nafasi, Omari Nundu, alisema
hatoweza kupeleka posa kwa watu hao kwani yuko na kimwana ambaye hasikii wala
haoni na ametua kwake.
Alisema hatokuwa tayari kupeleka
posa kwa wagombea hao wa nafasi ya Ubunge na Udiwani wa Chama Cha Wananchi
(CUF) kwani mke alienae amepoa licha ya ruhusa ya dini yake kuruhusu wake
wanne.
“Niko na kimwana anaenipendezesha na ndio maana nipo hapa na
kila mmoja ananifurahia----siko tayari kupeleka posa kwa watu hao kwani
nitakapotangazwa kuwa nimeshinda wote watakuja na kunipa mkono kwa heshima
zote” alisema Nundu
Nundu aliwataka wananchi kujitokeza
kwa wingi siku ya kupiga kura na kuwachagua wagombea wa CCM kwani kila alopewa
dhamana ya kugombea ameaminiwa na hivyo kuwapa kura nyingi za ushindi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment