Tangakumekuchablog
Dar es Salaam,
WAANDISHI wa habari wametakiwa kuzitumia kalamu zao kuwaelimisha wananchi juu
ya haki na wajibu wa kupiga kura na
kuacha kushabikia mambo ambayo hayana nafasi kwa jamii.
Akizungumza katika mafunzo ya siku
mbili yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na BBC
Media Group, mwandishi mkongwe nchini, Atilio Tigalile, aliwataka waandishi wa
habari kuzitumia siku zilizobaki kuandika habari nyingi za uchaguzi.
Alisema kuna baadhi ya vyombo vya
habari vimekuwa vikishabikia habari za upande mmoja na hivyo kuvitaka kuacha
kufanya hivyo na badala yake kuandika habari za pande zote mbili bila upendeleo
na kuzipa nafasi kubwa habari za uchaguzi.
“Ni jambo la furaha na faraja kuona
waandishi wengi mupo hapa kuzungumzia uchaguzi----niwatake kuandika habari kwa
weledi na usahihi bila kupendelea chama” alisema na kuongeza
“Hebu jamani tuzitumilieni siku hizi
chache kwa kuandika habari za uchaguzi
tena bila upendeleo----kuna vyombo vyengine hata havisemezeki wapo kwa ajili ya
mtu mmoja tu na huko itakuwa ni kukiukwa kwa maadili” alisema
Akizungumzia kuhusu wamiliki wa
vyombo vya habari TV na magazeti ,
Tigalile aliwataka kuandika makala kwa wingi kuelimisha wananchi juu ya wajibu
wa kupiga kura .
Alisema kuna kundi kubwa vijijini
bado elimu ya kupiga kura haijawafikia na hivyo kuvitaka kuandaa makala mfululizo
pamoja na habari katika siku chache zilizobaki.
“Sote tunatambua kuwa wananchi wa
mashamba na vijijini ni wafungwa wa kupata habari hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu October
25’ alisema na Tgalile
Alisema mwandishi makini ni yule
ambaye habari yake anaifanyia kazi na
kuuliza watu zaidi ya watatu na
kudai kuwa huo ndio ni uandishi mahiri
na makini ambaio hauvunji maadili.
No comments:
Post a Comment