Thursday, October 1, 2015

WANAJESHI 11 WA MAREKANI WAUWAWA AFGHANSTAN

Wanajeshi wa US wafariki ajali ya ndege Afghanistan

  • Hercules
Watu 11 wamefariki baada ya ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya Hercules kuanguka katika uwanja  wa ndege nchini Afghanistan, jeshi la Marekani limesema.
Ndege hiyo muundo wa C-130 ilianguka mwendo wa saa sita usiku katika uwanja wa ndege wa Jalalabad.
Kanali wa jeshi la Marekani Brian Tribus ameiambia AFP kwamba sita kati ya waliouawa walikuwa wanajeshi wa Marekani, na waliosalia walikuwa raia.
Ndege za muundo wa C-130 hutumiwa na jeshi kusafirisha wanajeshi na mizigo mizito.
Msemaji wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahid alisema kupitia Twitter kwamba kundi hilo lilitungua ndege hiyo, lakini mashirika ya habari yanasema hakuna ishara kwamba hilo lilikuwa shambulio.
Jeshi la Marekani limesema linachunguza kilichosababisha ajali hiyo.
Ajali hiyo ya ndege imetokea huku ndege za kijeshi za Marekani zikisaidiana na wanajeshi wa Afghanistan kujaribu kukomboa mji wa Kunduz uliotekwa na wapiganaji wa Taliban.
Takriban wanajeshi 10,000 wa Marekani wamo Afghanistan baada ya mpango wa kuondoa majeshi hayo asteaste kubadilishwa mapema mwaka huu.
Rais Obama alikuwa ameahidi kuacha wanajeshi wachache sana wa Marekani nchini humo ambao wangekuwa wa kulinda ubalozi wa Marekani kufikia mwisho wa mwaka 2016.
Chanzo BBC
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment