Mauaji mengine ya wanafunzi wakiwa chuoni Marekani, maneno ya Obama pia yapo hapa..
Polisi walipata taarifa hiyo baada ya mtuhumiwa huyo kufanya tukio hilo na kufika eneo la tukio..pia polisi walifanikiwa kumuua Harper Mercer ambaye anatuhumiwa kufanya mauaji hayo kwa kumpiga risasi akiwa bado eneo la tukio.
Mmoja wa mashuhuda ambaye alikua baba wa mmoja wa wanafunzi waliojeruhiwa alisema kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Harper Mercer kabla ya kufanya mauaji alikua akiwauliza watu hao wanatoka dini gani kisha kuwafyatulia risasi.
Polisi bado wanaendelea na uchunguzi kujua muuaji huyo alikua na lengo gani na kutafuta nyumba aliyokuwa akiishi.
Rais wa Marekani Barak Obama amesema matukio ya watu kuua raia yamekuwa yakawaida sana na kuvitaka vyombo husika kuweka sheria ya udhibiti wa silaha za moto.
Obama akizungumza baada ya tukio hilo…
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment