Waziri Abdallah Kigoda amefariki akiwa kwenye Matibabu India, Serikali imethibitisha hii..
Kulikuwa na taarifa nyingi zilizosambazwa Mitandaoni kuhusu hali ya Kiafya ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda
lakini Serikali ikakanusha kuhusu taarifa hizo na kutaarifu kuwa Waziri
huyo ni mzima hajafariki, ila alikuwa India bado akiendelea kupatiwa
Matibabu.
Taarifa iliyoripotiwa muda mfupi uliopita na kuthibitishwa na Serikali inahusu Msiba wa Waziri huyo, Abdallah Omar Kigoda ambaye alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.
Hiyo ni taarifa kutoka Ofisi ya Bunge
ikionesha Waziri huyo amefariki leo Jioni katika Hospitali ya Appolo
ambako alikuwa akitibiwa.. Serikali iko kwenye Mipango ya taratibu za
kusafirisha Mwili wa Marehemu pamoja na Mazishi kwa kushirikiana na
Familia ya Marehemu.
“Serikali inasikitika kutangaza kifo cha Dk. Abdallah Kigoda
aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kilichotokea Hospitali ya
Appolo India leo.. Taarifa kuhusu kusafirisha mwili wa Marehemu na
Mazishi mtaendelea kupatiwa. Dk Kigoda alilazwa tarehe 18 September 2015 ambako alikuwa akipatiwa matibabu” >>> Assah Mwambene,
No comments:
Post a Comment