Monday, October 12, 2015

KAPANGE WA CCM HAACHI VITUKO NAE



Tangakumekuchablog
Tanga, KATIBU wa Itikadi na Uenezi CCM Wilaya ya Tanga, Lupassio Kapange  haachi vituko vyake kila siku ya mikutano wa kumnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Tanga mjini CCM, Omari Nundu na jana ametoa kali kuwa upinzania ni tumbo la kuharisha.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni wa kumnadi , Omari Nundu kata ya Msambweni,  Lupassio aliwataka wananchi kuchagua CCM kwani ndio chama pekee ambacho kiko na uwezo wa kuwaletea maendeleo .
Alisema upinzani ni sawa na tumbo la kuharisha hivyo yoyote ambaye atakichagua ni sawa na tumbo la kuharisha ambalo hakutokuwa na kazi zaidi kupanga foleni hospitali kutaka matibabu.
“Ndugu zangu wananchi wa kata ya msambweni chagueni CCM kwani upinzania ni sawa na tumbo la kuharisha---ambalo muda wote liko hospitali kutaka matibabu” alisema Kapange na kuamsha vifijo
Alisema upinzania bado hawajajipanga na kuwa bado kushindana na CCM hivyo kurudi kwanza kujadiliana ndio warudi kuona kama wanaweza kupambana na  CCM.
Alisema upinzani hawajajipanga na ndio maana kila siku kunatokea mitafaruku wakati CCM ni mbele kwa mbele na kiko karibu na wanachi hivyo kuwataka kumchagua Omari Nundu amalize malengo yake.
Alisema Nundu yuko na uzoefu wa uongozi na wakati wa miaka mitano ya Ubunge wake aliweza kufanya mengi ikiwemo kutoa mikopo kwa wajasiriamali na fursa kwa vijana.
Alisema mgombea huyo ameweka malengo ya miaka mitano ijayo kuhakikisha kila kijana anafanya kazi kwani sera ya ufufuaji wa viwanda Tanga unaendelea ikiwa na pamoja na vile ambavyo vinafanya kazi vinatoa nafasi kwa wenyeji.
Aliwataka wananchi kumpa kura nyingi Omari Nundu na kuwa Mbunge wao na hivyo kuacha kuchagua upinzani kwa madai kuwa ni tumbpo la kuharisha na linaweza kuambukiza kila mtu.
                                             Mwisho

No comments:

Post a Comment