Mkazi wa Magaoni B mtaa wa Shule
akipita kwa shida nyumbani kwake baada ya maji kuzingira nyumba yake kufuatia
mvua kubwa iliyonyesha juzi usiku na maji hayo kutokuwa na njia ya kupitia na
kuingiwa na hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya miripuko ukiwemo wa kipindupindu
ambacho kimepiga hodi Tanga.
Kufuatia mvua hizo zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo kumesababiasha baadhi ya familia kuzihama nyumba zao na kukimbilia maeneo mengine kuokoa maisha yao na mali zao.
Wakizungumza na Mwandishi wa Tangakumekuchablog aliepiga hodi mtaani hapo, walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiiomba Serikali kuwachimbia mifereji ya maji lakini hadi hadi leo hii amedai hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Walisema majengo yao wamejenga kwa kufuatia sheria za jiji ikiwa na pamoja na kugaiwa viwanja na mipango miji lakini cha kuchangaza mamlaka hizo kudai hazikuzingatia sheria za mipango miji ya kuchima mifereji na maeneo ya wazi ili likitokea janga iwe rahisi kujiokoa.
No comments:
Post a Comment