WAJUMBE
wa Baraza la Wawakilishi wa Chama chama Wananchi (CUF)wamepinga matokeo
ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kufutwa kutokana na mtu
aliyefanya utenguzi huo ni utashi wake na sio Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC).
Wajumbe
27 wa baraza hilo wamewasili jijini Dar es Salaam kuzungumza na
waandishi wa habari juu ya kizungumkuti cha matokeo ya uchaguzi kufutwa
huku wakiwa wenyewe hatambui hatua hiyo.
Akizungumza
mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Abbakari Khamisi amesema
uchaguzi wao uliofutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),
Jecha Salum Jecha hawatambui na wataka waendelee kuhesabu kura hizo na
sio kurudia uchaguzi.
Amesema
uchaguzi utafutwaje wakati wajumbe wa baraza la wawakilishi wamepata
udhibitisho wa maandishi wa kushinda majimbo yao na kufanya uchaguzi
ukirudiwa ni ukiukwaji kwa katiba.
Khamisi
amesema kuwa uchaguzi wa Zanzibar, kushinda kwa Chama cha Mapinduzi
(CCM) ni halali na kushinda chama kingine kati uchaguzi unaonekana
batili huku wakujua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
“Hatutaki
uchaguzi urudiwe kwani kufanya hivyo ni kukiuka kwa katiba ya uchaguzi
kutokana na waangalizi walisema uchaguzi ulikuwa wa haki na huru kwa
nini urudiwe wakati katiba haina tafsiri ya kufuta na matokeo na
kufanyauchaguzi mwingine”amesema Khamisi.
Nae
Ismail Jussa mshindi wa jimbo la Marindi amesema kuwa hawatambui
kuendelea kwa utawala uliopo sasa kutokana na katiba ya Zanzibar.
Aliongeza kuwa nchi ya Zanzibara haina Rais na kufanya kuendelea kwa Rais aliyemaliza muda wake ni kukiuka kwa katiba.
Naibu
katibu mkuu wa Chama Cha wananchi CUF, Nassor Ahmed Mazrui akizungumza
na waandishi wa habari leo katika mkutano wa waandishi wa habari leo
kuhusiana na wabunge wa baraza la wawakilishi Zanzibar kumwomba rais wa
jamhuri ya muungano kuwaapisha ili waanze kufanya kazi yao kwaajili ya
kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao.
Mgombea
wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Abubakari Khamis akionyesha fomu ya
uthibitisho kuwa amechaguliwa kuwa mwakilishi wa baraza la wawakilishi
Zanzibar leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jana
jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wawakilishi waliochaguliwa kuwakilisha baraza la wawakilishi
Zanzibar waliohudhilia katika mkutano na waandishi wa habari jana jijini
Dar es Salaam.
Naibu katibu mkuu wa Chama Cha wananchi CUF, Nassor Ahmed Mazrui, akizungumza na waandihi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi
ya wajumbe wa bunge la wawakilishi Zanzibar wakionyesha fomu zao za
Ushindi wa walipohudhulia mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana.
chanzo glog ya jamii
No comments:
Post a Comment