Tangakumekuchablog
Tanga, JESHI la
polisi Mkoani Tanga linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuingiza nchini
madawa ya kulevya aina ya mirungi kilo 530 yakitokea Mombasa nchini Kenya kwa
kutumia kampuni ya usafirishaji abiria (Smart Bus).
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana, Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, alisema
kukamatwa kwa watu hao ni taarifa za wasamaria wema kuliambia jeshi la polisi
juu ya kuingiza madawa hayo.
Aliwataja watu hao kuwa ni, Mohammed
Omary (32), Haruna Hassan (35) na Aziz Othman (27) wote wakiwa wenyeji wa Tanga
na kusema kuwa taarifa za wasamaria wema zilifanikiwa kuwakamata.
“Taarifa za wasamaria wema kwa
kushirikiana na jeshi la polisi tuliweza kuikamata mirungi ikiwa imefichwa
uvungu wa basi juu ya vyuma----ni vigumu kugundua mara moja” alisema Mombeji na
kuongeza
“Hawa vijana ni hatari sana wameficha
mirungi kilo mia tano na thalathini----ni mingi sana ila tumeikamata na watuhumiwa
tutawakomesha na kuwa funzo kwa wengine” alisema
Alisema watuhumiwa hao wanahojiwa na
polisi na mara baada ya kukamilika kwa ushahidi watafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazowakabili na kuwa mfano kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Akizungumza kuhusu usalama wa
mipaka, kamanda Mombeji alisema kwa sasa wamezidisha doriia katika mpaka wake
na nchi jirani kuzuia mianya ya upitishaji wa wahamiaji haramu na mali za
magendo.
Alisema awali wahalifu walikuwa
wakiitumia mipaka hiyo kwa kupitisha wahamiaji haramu kutoka Ethopia na Somalia
pamoja na mali za magendo lakini kwa sasa wamezidisha ulinzi maradufu.
“Tumezidisha ulinzi katika mipaka
yetu kuzuia upitishaji wa wahamiaji haramu na mali za magendo----wahalifu
walikuwa wakiitumia vibaya na sasa
tutakula sahani moja” alisema kamanda Mombeji
Aliwataka wananchi kushirikiana na
jeshi hilo kwa kupeana taarifa za matukio mara kwa mara na kuacha kushirikiana na wahalifu kwani wataweza kuwaingiza katika
matatizo ambayo hawana matarajio nayo
Mwisho
Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji akiwaonyesha waandishi wa habari na maofisa polisi mirungi kilo 530 iliyokamatwa katika basi la abiria lililokuwa likitokea Mombasa nchini Kenye .
Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji akiwaonyesha watuhumiwa wa kuingiza mirungi kilo 530 kutoka Mombasa Kenya kwa waandishi wa habari wa Tanga jana nje ya Ofisi yake. Chini ni viroba vya mirungi vikiwa vimetawanywa
No comments:
Post a Comment