Tangakumekuchablog
Tanga POLISI
Mkoani Tanga imewakamata wahamiaji haramu 34 wenye asili ya Kiethopia wakiwa
wamefichwa kwenye Lori lililokuwa limebeba maji ya chupa ya Kilimanyaro
wakisafirishwa kuelekea Tunduma Mkoani
Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari , Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, alisema tukio hilo
lilitokea juzi saa 8 usiku kwenye kizuizi cha polisi cha Mazinde kata ya Kisiga
Wilayani Korogwe Tanga.
Alisema polisi wakati wakilikagua
gari hilo ambalo lilikuwa limesheheni katoni za maji katikati ya tela kulikuwa
na uwazi ambao ulitandikwa majamvi na magunia jambo ambalo amedai kuwa si
rahisi kugundua.
Alisema lori hilo ambalo lilikuwa
likielekea Tunduma Mkoani Mbeya lilikuwa limejaza maji na kuwa vigumu
kuwatatambua na wakati wa ukaguzi wa gari walisikia sauti za watu wakizungumza
na kukohowa.
“Wakati
wa upekuzi wa lile lori
lilikuwa limesheheni katoni za maji aina ya Kilimanjaro----dereva
alishuka kwa kasi na kutokomea porini na kushindwa kumkamata” alisema
Mombeji na kuongeza
“Haikuwa rahisi kuwagundua kwani gari
lilikuwa limesheheni katuni za maji hadi juu ----kilichosaidia wakati polisi
akiichunguza mipira sauti zilisikika ndipo alopopanda juu na kuona kundi la
watu” alisema
Alisema wakati wa mahojiano dereva
alikimbia mbio na kubaki utingo peke
yake ambapo kwa sasa anashikiliwa na polisi pamoja gari na mara baada ya
uchunguzi kukamilika atapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Katika tukio jengine, Kamanda
Mombeji aliwaambia wanahabari kuwa polisi Kabuku inamshikilia , Salim
Mgazi mkazi wa Usagara kwa tuhuma za kukutwa na mirungi kilo 12 ambayo alikuwa
ameificha katika begi lake lililokuwa na nguo.
Alisema tukio hilo lilitokea juzi
saa 11 jioni katika kizuizi cha polisi
cha Kabuku barabara Segera Chalinze kwenye basi la Tahmeed ambalo lilikuwa
linatokea Mombasa kwenda Dar es Salaam.
Alisema polisi wakati wa ukaguzi
wake wa gari na mizigo ndani ya buti na ndani ya gari ilifanikiwa kukuta
mirungi iliyofichwa katika begi la nguo ambayo ilikuwa izungushiwa mfuko wa
nailoni.
“Polisi wakati akikagua mizigo ndani
ya buti na ndani ya gari ilifanikiwa kuikuta mirungi kilo kumi na mbili katika
begi la abiria” alisema Mombeji
Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano
na jeshi la polisi katika kutokomeza matukio
ya kihalifu pamoja na upitishaji wa wahamiaji haramu na mali za magendo ambapo
amedai kuwa kuna baadhi ya wakazi wa mpakani wamekuwa wakishirikiana na
wahalifu.
No comments:
Post a Comment