Thursday, November 26, 2015

VUTA SIGARA CHINA HADHARANI UKIONE CHA MTEMA KUNI

Ukivuta sigara China hawakuachi, ndani ya miezi mitano imekusanywa faini ya mamilioni !!


Ishu ya kupiga vita uvutaji wa sigara hadharani imekuwa ikigusa headlines kwenye nchi mbalimbali… kuna athari pia ambayo mtu akikutana na moshi wa sigara anayapata, hiyo ndio sababu iliyofanya nchi kama Uingereza waweke sheria kudhibiti uvutaji sigara hadharani !!
China nao hawako nyuma… June 2015 walipitisha sheria kuzuia uvutaji sigara kwenye maeneo ambayo kuna watu, ukikamatwa ni faini, kifungo au vyote viwili kwa wakati mmoja.
Sasa ninayo ripoti ambayo imenifikia kuhusu kiasi cha pesa kilichokusanywa ndani ya miezi mitano tangu siku ambayo sheria yao mpya imepitishwa June 2015, unaambiwa kiasi cha pesa kilichokusanywa ni kama dola 89,230 ambazo kwa TZ inagusa kama Milioni 192 hivi, hiyo ni faini tu.
Kwenye maeneo ambayo ukinaswa unavuta hakuna msamaha ni kama mahotelini, maofisini, migahawani, na kwingineko ambako kunakuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu !Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment