Sunday, November 15, 2015

WANAOWANIA TUZO YA BBC HADHARANI

Majina matano ya wachezaji wa Afrika wanaowania tuzo ya BBC 2015 na rekodi ya waliotwaa tuzo hiyo 2000-2014


Ikiwa ni wiki kadhaa zimepita toka shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF litangaze majina ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika, November 14 shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) na lenyewe limetangaza majina matano ya wachezaji wa Afrika wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2015.
Manchester-City-v-Crystal-Palace
Yaya Toure
BBC imetaja majina matano yatakayowania tuzo hiyo miongoni mwa majina hayo matatu ni kutoka katika Ligi Kuu Uingereza, tuzo hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1992 uhusisha waandishi wa habari kuchagua kwa kupiga kura za wachezaji watakaoingia katika nominees  na baada ya hapo ndio watu wengine hupewa fursa ya kuchagua yupi anastahili.
Southampton-vs-Manchester-United
Sadio Mane
Hivyo nani sijui utapenda ashinde kwa kumpigia kura? haya ndio majina matano yaliotajwa kuingia katika kipengele hicho, Pierre-Emerick Aubameyang kutokea Gabon ila anacheza katika klabu ya Borussia Dortmund ya UjerumaniAndre Ayew kutokea Ghana lakini anakipiga katika klabu ya SwanseaYacine Brahimi wa FC Porto lakini anatokea AlgeriaSadio Mane wa Senegal anachezea klabu ya Southampton na Yaya Toure kutokea Ivory Coast na Man City.
Porto-vs-Maccabi-Tel-Aviv
Yacine Brahimi
West-ham-v-Chelsea
Andre Ayew
1899-Hoffenheim-v-Borussia-Dortmund-Bundesliga
Pierre-Emerick Aubameyang
Namna ya kumpigia kura mchezaji bora wa Afrika wa BBC unaweza piga kura kwa kubonyeza hapa vote here au kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kutuma kwenda namba +44 7786 20 20 08
  • Tuma 1 kumpigia Pierre-Emerick Aubameyang
  • Tuma 2 kumpigia Andre Ayew
  • Tuma 3 kumpigia Yacine Brahimi
  • Tuma 4 kumpigia Sadio Mane
  • Tuma 5 kumpigia Yaya Toure
Rekodi ya tuzo hizo kuanzia mwaka 2000 hadi 2014
  • 2000 Patrick Mboma – Cameroon na Cagliari/Parma (Italia)

  • 2001 Samuel Kuffuor – Ghana na Bayern Munich (Ujerumani)

  • 2002 El Hadji Diouf – Senegal na Lens (France)/Liverpool (Uingereza)

  • 2003 Jay-Jay Okocha – Nigeria na Bolton Wanderers (Uingereza)

  • 2004 Jay-Jay Okocha – Nigeria na Bolton Wanderers (Uingereza)

  • 2005 Mohamed Barakat – Egypt na Al Ahly (Misri)

  • 2006 Michael Essien – Ghana na Chelsea (Uingereza)

  • 2007 Emmanuel Adebayor – Togo na Arsenal (Uingereza)

  • 2008 Mohamed Aboutrika – Egypt na Al Ahly (Misri)

  • 2009 Didier Drogba – Ivory Coast na Chelsea (Uingereza)

  • 2010 Asamoah Gyan – Ghana na  Sunderland (Uingereza)

  • 2011 Andre Ayew – Ghana na Marseille (Ufaransa)

  • 2012 Christopher Katongo – Zambia na Henan Construction (China)

  • 2013 Yaya Toure – Ivory Coast na Manchester City (Uingereza)

  • 2014 Yacine Brahimi – Algeria na Porto (Ureno)

  • 2015 ??????????
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment