Tangakumekuchablog
Tanga, MAMLAKA
ya Maji Tanga (Tanga Uwasa) imedai kukabiliwa na changamoto ya wizi wa
miundombinu na uchakavu wa mabomba pamoja na uharibifu wa chanzo cha maji.
Madai hayo yametolewa Leo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Joshua Mgeyekwa wakati wa kikao cha Wadau
kukusanya maoni kwa ajli ya mpango mkakati kwa mwaka 2015 -2020 na kusema kuwa
hali hiyo inarejesha nyuma jitihada ya mamlaka kusambaza maji hadi vijijini.
Alisema wizi wa mifuniko ya mashimo
ya maji taka na miundombinu ya ya maji imekuwa kikwazo cha kuyafikia malengo
hivyo kuwataka wadau kushirikiana na tatizo hilo ili kuweza kuyafikia malengo
mamlaka iliyojiwekea.
“Ndugu wadau tumekutana hapa sisi
kueleza ya kwetu lakini nanyi tutaka kusikia maoni yenu kwetu---changamoto
zinazotukabili nadhani hata nanyi zinawaathiri” alisema Mgeyekwa na kuongeza
“Kwa pamoja tushirikiane ili
kuiwezesha mamlaka kuyafikia malengo yake ya kuwafikishia maji safi wananchi
vijijini ambako kwa sasa ndio dira yetu” alisema
Alisema kutokana na mji kukua kwa
kasi na mahitaji kuwa makubwa, mamlaka inangalia kuwa na chanzo chengine cha
maji badala ya kutegemea kimoja ambacho kimekuwa kikihudumia maeneo mengi.
Alisema chanzo hicho cha Mabayani
kimekuwa kikikabiliwa na changamoto ya uharifu mkubwa ikiwa na pamoja na
ukataji miti na uchimbaji wa madini na kusababisha upungufu wa maji.
Alisema kumejitokeza wimbi la ukataji
miti na uchmbaji wa madini karibu na
chanzo cha maji na kusababisha upungufu mkubwa wa maji nyakati za
kiangazi hivyo kuwataka wadau kushirikiana na mamlaka ili kutokomeza wimbi
hilo.
“Uchimbaji wa madini na ukataji wa
miti karibu na chanzo cha maji limekuwa tatizo sugu----kwa muda mrefu tumekuwa
tukisema na kuweka ulinzi masaa ishirini na nne lakini bila na nyinyi hatuwezi
kufanikiwa” alisema Mgeyekwa
Mkazi wa Mikanjuni, Pitter Mohammed,
ameitaka mamlaka hiyo kuongeza vituo vya huduma kwa wateja ili kupunguza
msongamano na foleni kwenye ofisi ya ulipaji ndani ya mamlaka hiyo.
Alisema jiji zima liko na vituo
viwili vya huduma kwa wateja jambo ambalo inakuwa kero wakati wa ulipaji wa
Ankara mwisho wa mwezi na kusababisha foleni kubwa na kuwa kero.
Alisema ili kuweza kufanikisha malengo
ya mamlaka ya maji iliyojiwekea, Mgeyekwa aliwataka wananchi na wadau wa maji
kushirikiana na mamlaka hiyo katika kuendeleza utoaji wa huduma nzuri.
Mwisho
Picha nambari DSCN1623jpg hadi picha
nambari DSCN1627jpg, Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita akizungumza katika
kongamano la wadau wa maji (Tanga Uwasa) lililofanyika juzi Tanga.
Mkazi wa Mikanjuni kata ya Mabawa Tanga, Pitter Mohammed akizungumza katika kongamano la wadau wa mamlaka ya maji safi Tanga (Tanga Uwasa) lilifanyika leo.
M ganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita akizungumza katika kongamano la wadau wa maji (Tanga Uwasa) lililofanyika Leo Tanga.
No comments:
Post a Comment