Saturday, November 14, 2015

TAIFA STAR V/S ALGERIA



Dk 21, Samatta anapata pasi nzuri ya kisigino, anaingia na kupiga shuti kali linagonga mwamba wa juu au mtambaa wa panya na kutoka nje

Dk 19, kapombe anapiga mpira mzuri wa adhabu unaingia katika eneo la lango la Algeria, mpira unamkuta MUdathir naye anapiga shuti kuuuubwaaaaaaaa

Dk 17, bado Algeria wanaonekana kutumia zaidi mbinu ya kupoteza muda ambayo kwa kiasi fulani wanaweza kufanikiwa kwani wanapunguza kasi ya Stars ambayo walianza nayo

Dk 13 hadi 15, wachezaji wa Stars wananaswa na mtego wa kuotoa wa Algeria. 

Dk 11 na 12, Waalgeria wanaonekana kupoteza muda kwa makusudi na inaonekana waamuzi bado hawajagundua ujanja wao

Dk 10 Bentaleb anaingia vizuri katikati ya lango la Stars lakini anapiga dhuti mtoto, Barthez anadaka kama uji
Dk 8, Ulimwengu anaambaa na mpira kutoka 18 ya Stars hadi 18 ya Algeria lakini anapiga shuti kuuubwaaaaa.

Dk 7, Cannavaro anafanya kazi ya ziada kuokoa, inakuwa kona na Algeria wanapiga haina madhara
Dk 5, Algeria wanaonekana kuanza kucheza taratibu na kuipa wakati mgumu Stars
Dk 3, Samatta anampiga beki chenga na kutoa pasi nzuri kwa Maguri lakini anaugonga mpira mbali na kipa anauwahi

Dk 2 Ulimwengu anatoa pasi nzuri kabisa inayomfikia Mbwana Samatta, yeye na lango anapaisha juuu kabisa
KIKOSI KAMILI HIKI HAPA:
Ally Barthez, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Himid Mao, Thomas Ulimwengu, Mudathir Yahya, Elius Maguli, Mbwana Samatta na Farid

No comments:

Post a Comment