Shirika la ndege Kenya lagoma kuipeleka timu ya taifa ya Kenya kucheza na Cape Verde …
Ikiwa timu ya Taifa ya Tanzania ipo Algeria tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi dhidi ya timu ya taifa ya Algeria katika mji wa Blida uwanja wa Mustapha Tchaker Jumanne ya November 17, majirani zao wa Kenya bado wanaripotiwa kukwama uwanja wa ndege kwa muda sasa.
Timu hiyo ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeshindwa kusafiri kuelekea Cape Verde na kukwama katika uwanja wa ndege wa Wilson
baada ya kampuni ya ndege iliyokuwa inatajwa kuingia makubaliano ya
kuisafirisha kugoma kuruhusu ndege hiyo iondoke hadi wakamilishiwe
malipo yao yote kwani hawana imani na shirikisho la soka la Kenya KFF kama litalipa deni.
Harambee Stars ambao wanapaswa kwenda Cape Verde kucheza mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 Urusi dhidi ya Cape Verde baada ya mchezo wa awali uliochezwa Kenya na Harambee Stars kuibuka
na ushindi wa goli 1-0, wanakabiliwa na ukata kwa muda sasa hata awali
waliripotiwa wachezaji kudai malimbikizo ya posho zao.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment