Friday, November 20, 2015

SIKU YA UVUVI DUNIANI, TANGAMANIO TANGA



Tangakumekuchablog
Tanga, KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt Yohana Budeba, ameziagiza mamlaka zinazohusika na uvuvi baharini kuchukua hatua kukomesha uharibifu wa mazingira na uvuvi   haramu wa utumiaji wa mabomu na mabomu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Siku ya Uvuvi Duniani iliyofanyika Kitaifa Mkoani hapa , Budeba amesema uvuvi haramu wa aina yoyote unatakiwa kukomeshwa na kuwachukulia hatua kali watu wenye kuendesha uvuvi huo.
Amesema viumbe hai vingi baharini vimetoweka hivyo kuzitaka mamlaka zenye kusimamia bahari kuhakikisha inakomesha ikiwa na pamoja na kuwapeleka katika vyombo vya sheria wenye kuendesha uvuvi huo.
Akizungumzia wavuvi kuvua kwa teknolojia ya kisasa, Katibu huyo aliwataka kuwa na vifaa vya kisasa ili uvuvi wao uwe wenye tija ambao utawawezesha kuwa wavuvi wakubwa na wa kisasa.
Amesema uvuvi wa mazoea umepitwa na wakati hivyo kuwataka kusoma na kuondokana kero ya kukimbizana na askari  wa baharini .
Amewataka wavuvi kuwa na mahusiano na viongozi wa mazingira na uvuvi ikiwa na pamoja na kupena taarifa za wavuvi wanavyokabiliana na changamoto za baharini.
                                                Mwisho



Afisa Mfawidhi Kituo cha Ukuzaji Viumbe maji Tanga, Omari  Ali akimueleza ufugaji wa samaki Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt, Yohana Budeba wakati wa Siku ya Uvuvi Duniani yaliyofanyika kitaifa Tanga jana Uwanja wa Tangamano.


 Afisa Mfawidhi  Kituo cha Ukuzaji Viumbe maji Tanga, Omari Ali, akimuonyesha majongoo ya baharini Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt Yohana Budeba wakati wa Siku ya Uvuvi Duniani yaliyofanyika uwanja wa Tangamano Tanga jana.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt Yohana Budeba, akiangalia samaki aina ya mfano wa Bunju wakati wa Siku ya Uvuvi Duniani yaliyofanyika Kitaifa Uwanja wa Tangamano Tanga jana.

No comments:

Post a Comment