Monday, November 9, 2015

TASWIRA YA JICHO LA TANGAKUMEKUCHABLOG (NGAMIANI TANGA)



Mkazi wa barabara ya 8 makutano ya barabara ya Jamaa na Maua Ngamiani Tanga, Suleiman Khalfani akishangaa chemba ikitiririsha maji machafu yenye kutoa harufu kali na kuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo na wapita njia.
Jiji la Tanga limekuwa katika changamoto ya kupambana na kero za mazingira ikiwemo machemba yanayozibuka na kutoa maji machafu yenye harufu kali pamoja na mitaro ya maji yenye kuzibuka
Pia jiji hilo limekuwa likikumbwa na madampo kurundikana takataka hadi barabarani na wakati mwengine hadi katika makazi ya watu jambo ambalo watu wengi  wamedai kuwa ni kero ambayo haijapatiwa ufumbuzi.
Hata hivyo halmashauri ya jiji la Tanga limekuwa likifanya jitihada za kuhakikisha jiji hilo linakuwa katika mazingira mazuri iendanayo na hadhi ya jiji kwa kuweka sheria ndogondogo inayowabana waharibifu wa mazingira.






No comments:

Post a Comment