Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za
Taifa Bw. Allan Kijazi akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uongozi
kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi-usu kwa Mhifadhi Mussa Mandia katika
Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
……………………………………………………..
Shirika la Hifadhi za Taifa
limeanza rasmi kutumia mfumo wa jeshi usu kutoka ule wa kiraia katika
utendaji kazi wake ikiwa ni hatua mojawapo ya kuongeza ufanisi katika
shughuli za uhifadhi.
Jumla ya wahifadhi 40
walihitimu mafunzo ya Awamu ya kwanza ya kubadili mfumo wa utendaji kazi
kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu kwa kwa viongozi maafisa wa
ngazi ya kati “Transformation Leadership Course for Middle Cadre
Wardens” yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi hivi karibuni.
Mfumo wa utendaji kazi kwa
kijeshi-usu utalisadia shirika kuimarisha nidhamu ili kuboresha utendaji
kazi hasa katika nyakati hizi ambapo changamoto kuu ya ujangili
unaotumia silaha za aina mbalimbali za moto hasa za kivita inazidi
kushika kasi.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za
Taifa Bw. Allan Kijazi akikabidhi zawadi ya kuhitimu mafunzo ya uongozi
kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi-usu kwa Mhifadhi Prisca Lyimo katika
Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Faustine Masalu akiongea
wakati wa hafla ya ufungaji wa mafuzo ya kutoka mfumo wa utendaji kazi
wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Faustine Masalu akiongea
wakati wa hafla ya ufungaji wa mafuzo ya kutoka mfumo wa utendaji kazi
wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za
Taifa Bw. Allan Kijazi akiongea wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo
kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za
Taifa Bw. Allan Kijazi akifungua mafunzo ya awamu ya pili mafunzo
kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.
Wahifadhi waliohitimu mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala
wa TANAPA Bi. Witness Shoo akiwa na Wahifadhi wa kike waliohitimu
mafunzo ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Bw.
Allan Kijazi akikagua gwaride maalum la wahitimu huku akiongozwa na
Kamanda wa Gwaride hilo Mhifadhi Kelvin Nkulila.
Gwaride la wahitimu wa mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu likitoa heshima mbele ya mgeni rasmi.
Gwaride la wahitimu wa mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu likitoa heshima mbele ya mgeni rasmi.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment