Kabla ya Rais Dkt. Magufuli
kuzindua Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju aliomba Bunge
likubali kutenguliwa kwa kanuni za Bunge ili kuruhusu wageni kuingia
ndani ya Bunge hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akihutubia Bunge la Jamhuri kama
ishara ya kuzindua Bunge la 11.
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim
Majaliwa akitoa hotuba ya kuahirisha Bunge hadi mwezi Januari mwakani
baada ya Mhe. Rais kulizindua Bunge hilo.
Spika Job Ndugai akatoa amri ya
kuwataka wabunge hao kuwa watulivu na walipokaidi amri hiyo akatoa amri
ya kuwataka watoke nje ya ukumbu wa Bunge.
Baada ya Mwanasheria Mkuu kutoa hoja Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akawahoji wabunge.
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu
Lissu akiomba mwongozo wa Naibu Spika kwa kile alichodai kuwa kanuni
zimekiukwa.Hata hivyo, kiongozi huyo wa Bunge alitoa mwongozo na baadaye
alisitisha Bunge kuwaruhusu wageni kuingia kwenye ukumbi wa Bunge.
Baadhi ya wabunge wa upinzani wakiteta jambo wakati wageni wakiingia Bungeni.
Makamu wa Rais wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
wakifuatilia yanayojiri Bungeni.
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia
Ackson (kushoto), Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Jaji Othman Makungu, Jaji
Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman na Spika wa Baraza la
Wawakilishi Pandu Ameir Kificho wakiingia kwenye ukumbi wa Bunge huku
wakiongozwa na mpambe wa Bunge.
Baada ya viongozi hao kuwasili
kwenye ukumbi wa Bunge, wabunge wa Upinzani waliendelea kupiga meza na
kuimba, hali iliyofanya ukumbi wa Bunge ukose utulivu.
Viongozi mbalimbali wakiwemo
Marais wastaafu, wakuu wa vikosi vya majeshi ya Ulinzi na Usalama,
Maspika wastaafu, Watendaji Wakuu wa Serikali, Mawaziri Wakuu wastaafu
na wageni wengine wakisikiliza hotuba ya Rais.
Baadhi ya wakuu wa mikoa, viongozi wa dini na wageni wengine waalikwa wakimsikiliza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Wabunge wote wa upinzani wakatoka
nje ya ukumbi wa Bunge isipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT
Wazalende,Zitto Kabwe aliendelea kubaki ukumbini.
Wabunge walionesha kuridhishwa na hotuba ya Mhe. Rais Makufuli, wakipiga meza kuunga mkono hotuba hiyo.
Baada ya kukamilika kwa kazi hizo,
Mhe. Rais Magufuli akasindikizwa na wapambe wa Bunge kutoka nje ya
Bunge huku akiambatana na Spika wa Bunge Job Ndugai.
Baadhi ya Mabalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli (wa pili
kushoto) akiwa na Marais Wastaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili
kulia), Benjamin Wiliam Mkapa (kulia) na Alhaj Ali Hassan Mwinyi
(kushoto).
Mhe. Rais Dkt. Magufuli (wa tatu
kulia) akiwa na Spika wa Bunge Job Ndugai, Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia kwake) na Rais wa
Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) na Marais Wastaafu Alhaj
Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Amani Abeid Karume (kulia).
Picha na Hussein Makame-MAELEZO
No comments:
Post a Comment