Tangakumekuchablog
Tanga, KUFUATIA
kukatika na kuwaka umeme mara kwa mara jijiji Tanga, Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) limetoa ufafanuzi na kusema kuwa hiyo ni kutoka na uhaba wa waji
kutoka katika vyanzo vyake vya Kidato na Mtera.
Afisa Uhusiano Huduma kwa Wateja
Tanesco Tanga, Monica Mabada, ameiambia Tangakumekuchablo kuwa uhaba wa maji katika
chanzo cha Mtera na Kidato Shirika hilo linalazimika kufanya jitihada mbadala
ili huduma ya upatikanaji umeme uendelee.
Alisema kwa sasa Shirika la Umeme
Tanzania liko katika mchakato wa kuhakikisha kero kwa wateja wa majumbani na
viwandani inaondoka kwa kutafuta vyanzo vyengine hadi mabwawa hayo yatakapojaa
maji.
“Kukatika umeme mara kwa mara kama
unavyosema huwa mara nyingi mafunzi wako
kazini si usiku wala mchana----hitilafu za umeme mara nyingi hutokea usiku”
alisema Mabada na kuongeza
“Ukatikaji wa umeme ni mafundi wako
kazini na hakuna tatizo lolote zaidi ya kusema vyanzo vyuetu vimepungukiwa na
maji lakini sio kuwa ni tatizo la wateja kupatwa na kitisho” alisema
Akizungumzia miundombinu ya umeme,
Afisa huyo alisema kuna marekebisho ya vifaa katika Transfoma yake kubwa ya
Majanimapana na hivyo wako katika mchakato wa mwisho wa kukamilisha.
Alisema kumalizika kwa kubadilishwa
kwa kifaa hicho wakazi wa jiji la Tanga watakuwa na uhakika wa umeme maradufu
na hivyo kuwataka kuwa wavumilivu kipindi hiki cha mchakato wa marekebisho ya
miundombinu yake.
Mwisho
No comments:
Post a Comment