Tangakumekuchablog
Tanga,IMEELEZWA
kuwa sekta ya Maziwa nchini inakabiliwa
na changamoto nyingi ikiwemo ya elimu ya ufugaji na miundombinu ya ufikishaji maziwa viwandani.
Akizungumza katika kongamano la
Kimataifa la wafugaji wa ngombe wa maziwa na wafanyakazi lililofanyika leo
Tanga, Mratibu wa Miradi kutoka kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh, Chales
Tumaini, alisema wafugaji wengi wako na changamoto katika ufugaji wao.
Alisema wafugaji wengi hawana elimu
ya ufugaji wa ngombe wa maziwa na badala yake wamekuwa wakiendesha kwa mazoea
jambo ambalo limekuwa likiwarudisha nyuma kwenye sekta ufugaji ng'ombe wa maziwa.
“Sekta ya ufugaji wa ngombe wa
maziwa unakuwa kwa kasi barani Afrika---lakini kuna changamoto kubwa kwa
wafugaji hasa wadogo wadogo ambao hawana elimu ya kutosha ya ufugaji” alisema
Tumaini na kuongeza
“ Usafi pia ni moja ufugaji mahiri
na wengi wamekuwa wakitumia vyombo ambavyo sio rasmi na maziwa yakifika
kiwandani na kupimwa yanapungua ubora na mfugaji kupata hasara” alisema
Kwa upande wake Mkufunzi na Mshauri
wa wafugaji wa maziwa kutoka Uholanzi, Ciska Anema, aliwataka wataalamu wa
mifugo kuwafuata wafugaji mashambani.
Alisema wafugaji wengi wa mashamabani
hawana elimu ya ufugaji wa ngombe wa maziwa na badala yake wamekuwa wakifuga
kienyeji na kutopata faida na hivyo kuiona sekta hiyo haina tija.
Aliwataka wataalamu na wafanyakazi
viwandani kuwatembelea wafugaji wao na kuwaelimisha ufugaji mahiri ambao
utaweza kuwaongezea kipato na kuacha kusubiri maziwa viwandani.
“Wamiliki wa viwanda wanapaswa
kuwatembea wafugaji wao mashambani na kuwapa elimu nzima ya ufugaji ----hii
itawaongezea wingi wa upatikanaji wa maziwa na faida” alisema Anema
Alisema wafugaji wengi wako na
shauku ya kuendesha mradi wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa lakini wanashindwa
kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ya ufugaji.
, Mkufunzi na Mshauri wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka Uholanzi, Ciska Enema, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la wafugaji na wafanyakazi wa sekta ya maziwa lililofanyika Tanga leo
No comments:
Post a Comment