Ripoti kutoka mahakamani Nigeria kuhusu kesi ya Mchungaji T B Joshua…
Mchungaji wa Kanisa la Church of All Nations Nigeria, TB Joshua
na Wakandarasi wawili ambao wanakabiliwa na mashtaka ya uzembe
uliopelekea jengo la Kanisa hilo kuanguka na kusababisha vifo vya watu
116, leo wameshindwa kufika Mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili
kuhusu vifo vya watu hao.
Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu ya Lagos Nigeria baada ya tukio la kuanguka kwa jengo la kufikia wageni lililopo kwenye Kanisa la TB Joshua September 12 2014 na kupelekea vifo hivyo ambapo kati ya waliofariki, 81 walikuwa raia wa Afrika Kusini.
Katika Mashtaka yaliyofunguliwa
Mahakamani, Kanisa hilo limedaiwa kufanya ujenzi wa jengo hilo la
ghorofa sita bila kuwa na kibali cha kufanya ujenzi huo.
Kwa upande wa TB Joshua
wamekuwa wakijitetea kwamba sababu ya jengo hilo kuanguka inatokana na
ndege moja ambayo ilizunguka juu ya jengo hilo, muda mfupi baadae jengo
hilo likaanguka.. anaamini kuna hujuma zilizofanywa kwenye tukio hilo.
Kukosekana kwa T B Joshua
na wakandarasi hao kumelalamikiwa pia kwamba ni kitendo cha makusudi na
hakuna sababu yoyote ya msingi, japo mmoja wa wanachama wa Bodi ya
kanisa hilo alikuwepo Mahakamani…
Jaji wa Kesi hiyo pia ameonekana kukerwa
na kitendo hicho huku akisisitiza kwamba hatovumilia uzembe wa aina
yoyote utakaofanya kuchelewa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka December 11 2015 ambapo TB Joshua na wakandarasi wake wawili wanatakiwa kuripoti Mahakamani hapo, Lagos Nigeria.
No comments:
Post a Comment